
Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umehitimishwa jana katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Watu wenye ulemavu na wadau mbalimbali wa Serikali na Mashirika yasiyo ya Serikali walikusanyika kutoka kila pembe ya dunia kujadili hatua zilizopigwa katika kipindi cha miaka 20 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu, CRPD.
Mmoja wa waliohudhuria ni Bwana Kibaya Laibuta ambaye licha ya kupoteza uwezo wa kuona akiwa na umri wa miaka 24 alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi bado alifanikiwa kusonga mbele akamaliza masomo yake ya sheria na masomo mengine ya ngazi za juu na sasa miaka mingi baadaye ni Jaji katika Mahakama ya Rufaa ya Kenya. Siri yake ya mafaniko ndio hasa anaihamasisha kote duniani na anaiweka wazi katika mazungumzo yafuatayo na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa ili watu wengine wenye ulemavu wafanikiwe kama yeye.
Nilipata usaidizi wa familia kuungwa mkono na familia na pia mashirika kama vile Kenya Society for the Blind. Nikamaliza chuo kikuu, nikaanza kazi yangu ya uwakili na hatimaye masomo ya ziada kule London (Uingereza) na kurudi tena kuendelea na kazi. Nimekuwa nikifundisha sheria katika vyuo vikuu viwili nchini Kenya na hatimaye nimefanya PhD yangu pale Chuo Kikuu cha Nairobi. Niseme kwamba ijapokuwa mtu anaweza kuwa na matatizo ya kuona ama ulemavu wa macho, kilicho muhimu ni uungwaji mkono wa programu tofauti tofauti. Vifaa vinavyo kusaidia katika masomo kuandika kama ‘mawasilisho yako ya kitaaluma’ ama kunakili program tofauti tofauti za mafunzo. Na hayo yote yamekuwa ni changamoto kweli manake vifaa hivi ni vya bei ghali. Lakini hata hivyo, inategemea pia uungaji mkono unaopata.
Je umepata nafasi ya kuwasilisha maoni yako katika mkutano wa 19 wa Nchi wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu?
Ndio tulikuwa na mjadala ambapo Kenya ilikuwa imeandaa mkutano, ulijaribu kuona jinsi gani ya vifaa vinavyohitajika na watu walio na ulemavu wa aina mbalimbali vinaweza kupatikana kuendeleza elimu tangu utotoni hadi kuendeleza elimu ya juu. Dunia ya leo iko katika mwendo wa ‘digital transformation’ na ni lazima kila mmoja ahusishwe na awe na uwezo pia wa ku access mifumo ya kidigitali ambayo ndio inayotawala. Hali ya kisasa. Kwa maoni yangu, serikali nyingi zimekua mashirika yasiyo ya Serikali ina jukumu la kushughulikia watu walio na ulemavu na sisi tunajua kwa uwazi kwamba ulemavu unakuja na gharama ya juu sana. Utakuta kifaa kidogo kinachosaidia kuandika kwa njia ya kidigitali utakuta ni shilingi nusu milioni (takribani dola elfu nne) na utapata kwamba kifaa hicho unaweza kukifananisha na kalamu ya wino ya mtoto aliye na asiye na matatizo ya kuona yatachukua kalamu watajiandikisha na yule mwanafunzi atapata pengine hata kwa senti kidogo za Dola ya Kimarekani, labda nusu dola. Hivi fikiria sasa hayo ndio matatizo inayokabili gharama ya juu zaidi. Kuna gharama pia ya kuhakikisha kwamba na kusomea vitabu ambavyo havijasajiliwa kwa njia ya digitali. Manake pia usipokuwa na hiyo mifumo ya kijiditali, hutaweza kupata kusoma vitabu hivyo kwa mtandao na pia unahitaji mtu wa kukuongoza kutembea na wewe. Hiyo ni gharama pia anahitaji malipo yake ya sasa.
Unafikiri tunatokaje hapo?
Lazima tuwe na nia na serikali, ishikilie mahitaji hayo ya kibinafsi pia kwa njia inayofaa ya kutenga fedha, kuhakikisha kwamba mifumo inapatikana ziko kwa wanaofanya kazi. Mashirika tofauti tofauti ya Serikali yanajaribu kuhakikisha kwamba wafanyakazi wao walio na mahitaji maalum. Kama sisi wanapata pia watu wa kuwashikilia kuhakikisha kwamba kazi zao haziwapi kulingana na elimu ambayo labda haikuwa. Kushughulikiwa kwa mifumo inayofaa, tutapata wengi walio na ulemavu wa aina mbalimbali. Wamebaki nyuma hawakupata elimu kamili kama wale walioweza kupata kazi nzuri. Imekuwa ni shida kwa.
Na ujumbe wake mahususi ni upi?
Niseme hivi. Ulemavu sisi si ukosefu wa nguvu za kutenda ama mawazo ama ni shida kwetu. Shida tu ni kupata jeans. Tuna viungo mkono kuhakikisha kwamba mahitaji yetu yanashughulikiwa inavyofaa.