Mchezaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ivory Coast, Amad Diallo, ameisaidia nchi yake kuanza vema michuano ya kombe la dunia baada ya kufunga goli pekee lililowapa ushindi tembo la Ivory Coast dhidi ya Ecuador.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Diallo ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Bazoumana Toure, aliifungia timu yake bao la ushindi katika dakika ya tisini ya mchezo, bao ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo.

Ushindi huu unaifanya Ivory Coast kushika nafasi ya pili kwenye kundi E nyuma ya Ujerumani ambazo zote zina alama tatu, isipokuwa Ujerumani inaongoza kwa idadi ya mabao baada ya jana usiku kuwafunga Qurasao kwa magoli 7 kwa 1.

Wachezaji wa timu ya taifa ya tembo la Ivory Coast
Wachezaji wa timu ya taifa ya tembo la Ivory Coast AP Photo/Petr David Josek – Petr David Josek

Huu ushindi wa kwanza wa Ivory Coast kwenye Kombe la Dunia katika kipindi cha miaka 12, tangu walipoifunga Japani nchini Brazil mwaka 2014, na sasa wanaweza kuwa na uhakika wa kufika hatua ya mtoano katika mashindano ya mwaka huu kwa mara ya kwanza.

Wawakilishi wengine wa Afrika, timu ya taifa ya Tunisia, yenyewe ilianza vibaya michuano hii kama ilivyokuwa kwa Afrika Kusini, baada ya kupoteza kwa mabao 3 kwa 1 dhidi ya Sweden.

Mashabiki wa timu ya taifa ya Ecuador
Mashabiki wa timu ya taifa ya Ecuador REUTERS – Dylan Martinez

Timu ya taifa ya Morocco yenyewe angalau ilianza vizuri baada ya kutoa sare ya bao 1 kwa 1 na mabingwa mara tano wa kombe la dunia, Brazil.

Aidha baadae hivi leo, wawakilishi wengine wa Afrika, Cape Verde watacheza dhidi ya Uhispania, huku Misri wenyewe watakuwa na kibarua dhidi ya Ubelgiji, kuanzia saa moja usiku na saa nne usiku saa za Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *