EPL

Chanzo cha picha, EPL

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 4

Dirisha la usajili la majira ya kiangazi kwa msimu wa 2026/27 limefunguliwa rasmi likitoa nafasi kwa klabu England kufanya maboresho ya vikosi vyao kabla ya msimu mpya kuanza.

Usajili ukianza rasmi leo Jumatatu, tarehe 15 Juni 2026 kwa klabu za England, kwa upande wa ligi zingine kubwa ya Ulaya kama La Liga (Hispania), Serie A (Italia), Bundesliga (Ujerumani) na Ligue 1 (Ufaransa), dirisha la usajili linatarajiwa kufunguliwa mapema kati ya Juni 29-Julai 1, 2026.

Licha ya tofauti ya kuanza, ligi zote kuu za Ulaya zitafunga dirisha la usajili kwa pamoja siku moja, ambayo ni Jumanne, tarehe 1 Septemba 2026. Baada ya tarehe hiyo, vilabu havitaruhusiwa tena kusajili wachezaji isipokuwa kwa masharti maalum ya sheria za ligi husika.

Kwa klabu kubwa za England, ikiwa ni pamoja na Arsenal, Chelsea, Manchester City, Manchester United na Liverpool, dirisha la usajili la majira ya kiangazi ni zaidi ya vita ya kujiimarisha. Je zinahitaji nini na nani kuongeza nguvu?

Arsenal – Winga wa kushoto

c

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal walimaliza msimu uliopita kama mabingwa baada ya ukame wa miaka 22 lakini pia kufika fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya, lakini changamoto yao kubwa ilionekana kuwa ukosefu wa ubunifu wa moja kwa moja upande wa kushoto wa ushambuliaji.

Mashambulizi yao mengi yalitegemea upande wa kulia kwa Bukayo Saka, jambo lililowafanya wakati mwingine kuwa rahisi kusomwa na wapinzani.

Klabu hiyo sasa inatafuta winga wa kushoto mwenye kasi, uwezo wa kupiga chenga na kuingia ndani ya eneo la hatari kwa urahisi. Mchezaji anayehitajika pia anatarajiwa kuongeza mabao na pasi za mabao moja kwa moja.

Miongoni mwa wanaofuatiliwa ni Christos Tzolis wa Club Brugge, Morgan Rogers wa Villa, Bradley Barcola na Khvicha Kvaratskhelia wa PSG, Nico Williams wa Athletic na Eli Junior Kroupi, ambao wana sifa za kucheza kwa moja kwa moja na kuvunja safu za ulinzi.

Chelsea – Beki wa kati na kushoto

Maxi Araújo

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Chelsea walimaliza msimu uliopita katika nafasi ya 10 wakikosa kucheza michuano ya Ulaya. Wanaonekana kuwa na changamoto za kiulinzi, hasa katika kuhimili mashambulizi ya wapinzani katika mechi kubwa. Ukosefu wa uzoefu nyuma umechangia kuruhusu mabao muhimu.

Marc Cucurella anakwenda Real Madrid kwa ad aya £51.8m, anazidi kupunguza uzoefu, akisalia Jorrel Hato. Kiungo Enzo Fernandez naye mguu ndani mguu nje.

Walinzi Maxi Araújo (Sporting CP), Andrea Cambiaso (Juventus) na Lewis Hall wa Newcastle wanafuatiliwa kumriti Cucurella.

Klabu hiyo inahitaji pia beki wa kati mwenye uzoefu wa Ligi kuu ya EPL au ligi kubwa za Ulaya, anayeweza kuleta utulivu na uongozi katika safu ya ulinzi. Pia anapaswa kufaa katika mfumo wa mabeki watatu unaotarajiwa kuendelea kutumika chini ya kocha mpya, Xabi Alonso.

Manchester City – Kiungo wa kati

s

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Manchester City walimaliza nafasi ya pili kwneye ligi nyuma ya Arsenal, wakifanikiwa kutwaa makombe mawili ya FA Cup na Carabao Cup walikumbwa na changamoto ya kupoteza udhibiti wa baadhi ya michezo, hasa pale walipokosa kiungo wa kati anayeweza kuamua kasi ya mchezo. Hii ilifanya baadhi ya mechi kuwa wazi zaidi kuliko kawaida ya mfumo wao.

Wanamtaka kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson, wakati huu ambao Rodrigo Hernández Cascante, au Rodri kiwango chake kikishuka kutokana na majeraha na Bernardo Silva akitarajiwa kujiunga na Real Madrid.

Manchester United – Kiungo wa kati

s

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Manchester United walimaliza wa tatu msimu uliopita, Wamekuwa kwenye kiwango bora tangu Michael Carrick achukue mikoba ya kuwanoa mashetani hao wekundu. Lakini tatizo kuu likiwa katikati ya uwanja, hasa kiungo wa chini na kiungo wa kati. Bruno Fernandez amekuwa bora kwenye kiungo wa ushambuliaji, anahitaji nguvu ya kiungo mwingine bora wa kati.

Klabu inahitaji kiungo wa kati mwenye nguvu, kasi na uwezo wa kusaidia ulinzi na mashambulizi kwa pamoja kupunguza mzigo kwa nahodha Bruno.

Kiungo wa kibrazil, Ederson anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa £35 million kutoka Atalanta, muda wowote baad aya kombe la dunia. Inamfuatilia pia kiungo wa West Ham, Mateus Fernandes na beki wa kushoto akiwemo Lewis Hall wa Newcastle United.

Liverpool – Winga wa kulia

Yan Diomande

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Liverpool walipitia msimu mbovu na kufukuza kocha wake Arne Slot ikikosa kabisa uwezo wake wa kawaida wa ushindani kwenye ligi, huku pengo kubwa likionekana upande wa kulia wa ushambuliaji.

Mo Salah ambaye ameshaaga Liverpool hakuwa na msimu bora hivyo kocha mpya Andoni Iraola ameelekeza macho yake kwa Yan Diomande kutoka RB Leipzig ambaye ada yake inaweza kufikia £87million.

Hata hivyo italazimika kuingia sokono kusaka beki mwingine wa kati mzoefu baada ya Ibrahima Konaté kusaini mkata wa miaka minne Real Madrid. Mkorea wa FC Midtjylland, Lee Han-beom anatajwa kusakwa ili kumrithi Konaté

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *