
Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, mizani ya usawa wa kimataifa haiwezi kujengwa bila ya nchi yake na akaongeza kuwa majaribio ya kuitenga Russia katika miaka ya hivi karibuni yamefeli.
Putin ameyasema hayo katika hotuba yake ya kila mwaka aliyotoa kwenye Klabu ya Majadiliano ya Valdai mjini Sochi, ambapo amebainisha kwamba Russia imeunganishwa kwa njia isiyoweza kutenganishwa katika michakato mingi ya kiuchumi, kitamaduni na ya kiusalama ya kimataifa, na haiwezi kutengwa nayo kwa matashi ya mataifa ya Magharibi.
“Nadhani wale ambao wamejaribu kuyaharibu [mafungamano haya], wameshawishika na” ukweli huu, ameeleza Rais wa Russia.
Ameendelea kueleza kwamba majaribio ya kuitoa nchi yake katika mfumo wa kimataifa zimeshindikana kw sababu mfumo huo haiuwezi kufanya kazi bila kuwepo mhusika muhimu kama Russia.
Rais wa Russia amesisitiza kwa kusema: “Imetokea na kuthibiti kwamba mfumo uleule wa kimataifa ambao [baadhi] walitaka kutufukuza sisi, kututoa sisi nje, hauruhusu Russia iondoke, kwa sababu inahitaji Russia kwa kuwa ni sehemu muhimu sana ya kuleta usawa na mlingano wa ulimwengu”…/