MBUNGE wa Gairo, Ahmed Shabiby, ameutaka Serikali kupitia upya mfumo wa utoaji wa leseni kwa waendesha bodaboda, akieleza kuwa gharama za mafunzo na upatikanaji wa leseni ni kubwa na zinawaathiri vijana wengi wanaotegemea sekta hiyo kujipatia kipato.

Akichangia mjadala wa Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2026/27 pamoja na Bajeti ya Serikali ya mwaka 2026/27, Shabiby amesema waendesha bodaboda hulazimika kulipa takribani Sh100,000 kwa ajili ya mafunzo kabla ya kupata leseni, hali ambayo imekuwa kikwazo kwa wengi kuendesha shughuli zao kwa kufuata sheria.

Mbunge huyo amependekeza Polisi Kata wapewe jukumu la kutoa mafunzo na semina kwa waendesha bodaboda, kisha kuwapatia vibali vitakavyowawezesha kupata leseni bila kulazimika kuhudhuria mafunzo katika vyuo.

Aidha, ameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupunguza gharama za leseni za bodaboda kutoka Sh70,000 hadi Sh50,000 ili kuongeza idadi ya vijana wanaopata leseni na kuendesha biashara zao kwa mujibu wa sheria.SOMA: Usajili bodaboda, leseni za bajaji, guta wapunguzwa

Shabiby amesema hatua hizo zitasaidia kupunguza mzigo wa gharama kwa vijana, kuongeza utii wa sheria na kuchochea ukuaji wa sekta ya usafiri wa bodaboda, ambayo imeendelea kuwa chanzo muhimu cha ajira kwa maelfu ya Watanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *