Hatua mpya imepigwa katika mchakato unaoongoza kwa kura ya maoni inayowezekana ya kikatiba nchini DRC. Baada ya Bunge, Baraza la Seneti limepitisha siku ya Jumatatu, Juni 15, 2026, muswada unaoelezea taratibu za kufanyika kwa kura ya maoni. Hata hivyo, Maseneta walirekebisha muundo wa Bunge Maalumu la Katiba lililopewa jukumu la kuandaa mageuzi yatakayowasilishwa kwa kura ya wananchi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Pascal Mulegwa

Muswada huo ulipitishwa kwa kauli moja na maseneta 89 waliokuwepo kati ya wanachama 109 wa Braza la Seneti. Muswada huu unafafanua, kwa mara ya kwanza, taratibu za kufayika kwa kura ya maoni nchini DRC.

Muswada huu unachochea mvutano wa kisiasa: upinzani unaona kama mwanzo wa mabadiliko ya kikatiba ambayo, kulingana nao, yanaweza kufungua njia kwa muhula wa tatu wa Rais Félix Tshisekedi.

Lakini Baraza la Seneti halikupitisha kwa ukamilifu toleo lililopigiwa kura siku chache zilizopita na Bunge. Mbali na kubadilisha maneno katika baadhi ya vifungu, maseneta walianzisha marekebisho kuhusu muundo wa Bunge Maalumu la Katiba lililopewa jukumu la kuamua uwezekano wa Katiba mpya.

Madiwani wa manispaa, wakiwemo wabunge wa kitaifa, waliondolewa kwenye mfumo na Baraza la Seneti, ambalo linajumuisha maseneta, manaibu, na wajumbe wa mabunge ya mikoa pekee.

Upinzai una hofu yauwezekano wamuhua wa tatu wa Tshisekedi 

Ili kuhalalisha uamuzi wake, Baraza la Seneti lilielezea kwamba uchaguzi wa madiwani wa manispaa ulikuwa umepangwa tu katika miji mikuu ya mikoa, ukiondoa miji mingine nawilaya za vijijini.

Tofauti hii sasa inalazimisha mabunge yote mawili kuoanisha misimamo yao. Katika tukio la mzozo, kulingana na utaratibu, msimamo wa Bunge utashinda.

Muungano wa upinzani C64 unafutilia mbali mpango huu. Viongozi wake wanauona kama mbinu iliyokusudiwa kusafisha njia ya kupitishwa kwa Katiba mpya ambayo, kwa maoni yao, intamuwezesha Rais Félix Tshisekedi kugombea muhula wa tatu baada ya mwaka 2028.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *