
Rais wa Somaliland, Abdirahman Mohamed Abdullahi, amepokelewa siku ya Jumapili, Juni 14, 2026, mjini Jerusalemu, na mwenzake wa Israel, Isaac Herzog. Hii ilikuwa ziara ya kwanza rasmi ya kiserikali ya na mkuu wa nchi wa Somaliland nje ya nchi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkutano huu unakuja baada ya uamuzi wa Israel kutambua Somaliland kama “taifa huru na linalojitawala” mnamo Desemba 26, 2025. Hii ni mara ya kwanza katika wigo wa kimataifa tangu eneo hilo kujitenga na Somalia mnamo mwaka 1991. Siku ya Jumatatu, Juni 15, Rais wa Somaliland alizindua ubalozi mpya wa nchi yake huko Jerusalemu.
Rais Abdirahman Mohamed Abdullahi ambaye alipokelewa kwa heshima rasmi mjini Jerusalemu, aliishukuru Israeli kwa moyo mkunjuvu “kwa niaba ya wakazi milioni sita” wa Somaliland. Ziara hii, kulingana na mkuu wa nchi, inafungua “ukurasa mpya” na “ni muhimu sana,” alitangaza.
Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais Herzog, kiongozi wa Somaliland pia alibainisha kuwa maafisa wa nchi yake wamekuwa wakijaribu “kwa miaka 35 kuanzisha mawasiliano na viongozi kote ulimwenguni,” na kwamba ni Israel pekee iliyokubali “kuiona na kuitambua” nchi yake.
Kufuatia utambuzi huu, Somaliland ilimteua Mohammed Hagi kama mkuu wa ujumbe wake wa kidiplomasia nchini Israel mnamo Februari. Kisha, mwezi Aprili, Israel ilitangaza uteuzi wa balozi asiye mkazi wa Somaliland.
Ubalozi wa Somaliland wazinduliwa Jerusalemu
Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, uzinduzi rasmi wa ubalozi wa Somaliland nchini Israel ulifanyika siku ya Jumatatu, Juni 15, huko Jerusalemu. Huu ulikuwa mwisho wa ziara ya siku nyingi ya rais Abdirahman Mohamed Abdullahi, ambayo ilijumuisha mikutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Kwa upande wake, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud alisema katika mahojiano ya televisheni sku ya Jumamosi kwamba Somaliland iliangukia katika mtego uliowekwa na Israel, ambao unahatarisha kusababisha mvutano mkubwa wa kikanda.