Takriban nusu ya watoto wote duniani  sasa wanaishi katika mazingira yanayokabiliwa na hatari zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa, hali inayotishia afya yao, elimu na maisha yao kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo inaonesha kuwa karibu kila mtoto duniani anakabiliwa na tishio moja la kimazingira , huku watoto zaidi ya million 4 wakikabiliwa na hadi hatari sita zinazojitokeza kwa pamoja.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto ulimwenguni UNICEF, imesema Watoto wengi wanaathiriwa na mchanganyiko wa majanga ya hali ya hewa kama ukame, mawimbi makali ya joto, mafuriko na vumbi.

Mataifa kama vile Bangladesh, Myanmar na Pakistan yametajwa kuwa baadhi ya maeneo ambayo Watoto wanakubwa na hatari hiyo.

Hata hivyo shirika la UNICEF imezitaka serikali duniani, kuongeza uwekezaji katika huduma muhimu za kijamii kama afya, na elimu ili kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika mazingira yenye hatari nyingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *