Shirika la Msalaba Mwekundu limeonya kuwa mlipuko virusi vya  Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado haujafikia kilele chake, na kwamba unaweza kuchukua mwaka mmoja kudhibiti kuenea kwa maambukizi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na wanahabari kutoka mjini Bunia, kitovu cha mlipuko wa virusi vya Ebola, Bruno Michon, meneja wa operesheni zinazohusiana na mlipuko wa Ebola katika shirika la Msalaba Mwekundu, amesema imekuwa vigumu kubaini kiwango ambacho ugonjwa huo umeenea hadi kufikia sasa.

Afisa huyo amesema ili kudhibiti mlipuko huo, juhudi kubwa zinafaa kuwekwa katika kuelimisha jamii zilizoathirika na kupata ushirikiano wao.

Michon amesema kuwa katika siku za hivi karibuni, wafanyakazi wa kujitolea wa Msalaba Mwekundu huko DRC wamekabiliwa na matusi, vitisho na hata kushambuliwa walipokuwa wakifanya kazi yao.

Mlipuko huo wa aina adimu ya Bundibugyo hadi sasa umeua watu 192 nchini DRC, huku takribani watu mia nane wakiambukizwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *