Kylian Mbappe, Michael Olise na washindi wa Ligi ya Mabingwa Ousmane Dembele na Desire Doue wote wanaanza katika kikosi cha kwanza cha Ufaransa kilichojaa mastaa.

Beki wa Arsenal William Saliba anaanza baada ya kupona jeraha la mgongo, huku Rayan Cherki, N’Golo Kante na Bradley Barcola wakiwa miongoni mwa wachezaji wa akiba.

Kikosi cha kwanza cha Ufaransa: Maignan, Kounde, Saliba, Upamecano, Theo Hernandez, Tchouameni, Rabiot, Olise, Dembele, Doue, Mbappe

Kikosi cha Kwanza cha Ufaransa dhidi ya Senegal katika Kombe la Dunia la FIFA 2026

Chanzo cha picha, BBC Sport

Mkongwe wa Everton Idrissa Gueye alikosa mazoezi Jumamosi kama hatua ya tahadhari lakini yuko fiti kuanza kwa Senegal.

Nicolas Jackson anaongoza safu ya ushambuliaji, na mshambuliaji wa Crystal Palace Ismaila Sarr na nyota wa zamani wa Liverpool Sadio Mane wakikamilisha safu ya mbele ya Simba wa Teranga.

Kikosi cha kwanza cha Senegal: Edouard Mendy, Diatta, Koulibaly, Niakhite, El Hadji Malick Diouf, Camada, Idrissa Gueye, Pape Gueye, Ismaila Sarr, Jackson, Mane

Kikosi cha Kwanza cha Senegal dhidi ya Ufaransa katika Kombe la Dunia la FIFA 2026

Chanzo cha picha, BBC Sport

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *