Jukwaa la kisiasa linalojumuisha vyama vya upinzani vinavyopinga mpango wa kufanyika kwa marekebisho ya katiba nchini DRC la C64 sasa limeandaa maandamano ya nchi nzima tarehe 08 mwezi Julai, kumtaka rais Félix Tshisekedi kuondoka madarakani.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili la Jukwaa la C64 lilitolewa hapo jana siku ya jumanne baada ya kutamatika kwa mkutano wa viongozi wa vyama vya upinzani, mkutano uliolenga kutathmini matukio ya Juni 12, kuhusu mwitikio mkubwa wa maandamano yao yaligubikwa na vurugu jijini Kinshasa, ambapo watu kadhaa waliripotiwa kujeruhiwa miongoni delly sessanga na Martin Fayulu pamoja na wafuasi wao.

Maandamano haya mapya ya Julai 08 yanatarajiwa kufanyika Jijini Kinshasa mbele ya Ikulu ya rais Félix Tshisekedi kumtaka ajiuzulu, upinzani ukimtuhumu kwa uhaini na kutoilinda Katiba.

Promesse Matofali mwakilishi wa chama cha upinzani cha ensemble pour la République kutoka mashariki mwa DRC.

‘‘Huo ni utawala ambao ulitoka kwenye uchaguzi na inaonekana vuguvugu hili lina agenda moja na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.’’ Amesema Promesse Matofali.

Hata hivyo upande wa Chama tawala cha UDPS wao wamepuuzilia mbali juhudi hizi za upinzani. Lwanzo kasonia Jean de Dieu, ni mwakilishi wa chama hicho akiwa Kinshasa.

‘‘Tumeamua kuandamana tarehe nane mwezi Julai kwa sababu wakati wa kutoa ushauri wa Rais umefika na yeye hapendi kusikia.’’ Amesema Lwanzo kasonia Jean de Dieu.

Siku ya Jumatatu, Juni 15, Baraza la Seneti lilipitisha muswada unaoelezea taratibu za kufanyika kwa kura ya maoni, Maseneta walirekebisha muundo wa Bunge Maalumu la Katiba lililopewa jukumu la kuandaa mageuzi yatakayowasilishwa kwa kura ya wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *