Wakati Iran na Marekani zilipokuwa zinakaribia kufikia mapatano ya awali kuhusu kusimamisha vita, utawala wa Kizayuni kwa mara nyingine tena siku ya Jumapili (Juni 14, 2026) ulishambulia viunga vya mji wa Beirut, na hivyo kuendelea kukiuka usitishavi vita.

Esmail Baghai, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiashiria mapatano hayo na jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon amesisitiza kuwa: ‘Lebanon na kusimamishwa vita nchini humo ni sehemu muhimu isiyotenganishika na maelewano ya kusimamisha mapigano. Baadaye, itabainika wazi kuwa vitendo vya kigaidi vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon imekuwa fursa ya kudhamini zaidi maslahi ya kitaifa ya Iran, mhimili wa muqawama na Lebanon. Vizazi vijavyo vitaona kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na marafiki zake hawakuruhusu vitendo viovu vya utawala wa Kizayuni vivuruge mwelekeo wetu wa kudhamini maslahi makubwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Lebanon, na kwamba kwa hakika jinai hizo zilipelekea kuweko mshikamano na nguvu kubwa zaidi ya mrengo wa muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni.’

Matamshi ya Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaonyesha kuwa, umoja wa nyuga au nyanja una umuhimu mkubwa kwa Tehran, ambapo jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon pia zinaonyesha kuwa kuzuia kupatikana umoja huo kuna umuhimu mkubwa kwa utawala huo. Kuhusu suala hili, sababu kadhaa zinaweza kutajwa: Kwa mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, umoja wa nyanja na kuimarishwa uhusiano wake na wanachama wa Mhimili wa Mapambano ni jambo muhimu katika kuzuia kuvurugika mlingano wa nguvu za kieneo kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni. Bila shaka, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo wa kujilinda peke yake dhidi ya uchokozi wowote na imedhihirisha wazi uwezo huo katika vita vya siku 12 na 40. Kusaidia wanachama wengine wa Mhimili wa Muqawama kunamaanisha kuendelezwa nafasi chanya ya mhimili huu katika eneo la Asia Magharibi na pia taathira zake chanya katika kudumisha uwiano wa nguvu katika eneo.

Katika upande mwingine, na kwa mtazamo wa utawala wa Kizayuni, kuondolewa au kudhoofishwa mwanachama yeyote wa Muhimili wa Mapambano hususan Hizbullah ya Lebanon ni hatua muhimu katika kuvuruga mlingano wa nguvu kieneo kwa maslahi ya utawala huo. Kwa hiyo, katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, umejaribu kadiri unavyoweza kuvuruga mazungumzo kati ya Iran na Marekani, na wakati huo huo kujaribu kuzuia Lebanon isiingizwe katika makubaliano yoyote kati ya Tehran na Washington.

Sababu na nukta nyingine ni kwamba, utawala wa Kizayuni umeyakalia kwa mabavu maeneo ya kusini mwa Lebanon kwa muda wa miezi 18 iliyopita, na kuyahifadhi pia bila shaka ni muhimu kwa Tel Aviv. Kwa mujibu wa ripoti za kuaminika, kuondolewa askari wote wa Kizayuni katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Lebanon ni moja ya vipengele muhimu vya mapatano ya Iran na Marekani. Mahmoud Al-Qamati, mmoja wa viongozi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa “wanajeshi wa utawala wa Kizayuni lazima waondoke katika ardhi ya nchi hii.” Kwa hakika, kifungu hiki cha makubaliano ya Iran na Marekani kinaonyesha kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haioni umoja wa ardhi kama suala tu la kulinda uwiano wa nguvu kieneo, bali pia inauona kama sababu ya kuimarisha nafasi ya ndani ya Hizbullah nchini Lebanon ili baadaye iweze kuokomboa ardhi ya nch hiyo kutoka katika makucha ya utawala ghasibu wa Israel, iwapo serikali na jeshi la Lebanon litashindwa kufanya hivyo.

Kwa kutilia maanani sababu zilizotajwa, wachambuzi wa mambo, vyombo vya habari, wakosoaji na hata wajumbe wa baraza la mawaziri la Netanyahu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu wanaamini kuwa upande mkuu uliopata hasara na kudhurika zaidi na mapatano ya Iran na Marekani ni utawala wa Kizayuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *