Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz amesema nchi yake imekuwa ikishirikiana na kwa siri na jimbo la Somaliland kwa miaka mingi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katz ametoa kauli hii wakati alipokutana na Abdirahman Mohamed Abdullahi, rais wa jimbo hilo lililojitenga na Somalia.

Aidha, Katz amesema Israeli na Somaliland zina urafiki wa muda mrefu unaozingatia maslahi ya pamoja, maadili ya kidemokrasia, na kujitolea kwa usalama na utulivu.

Waziri huyo wa usalama wa Israel, amesisitiza kuwa mataifa hayo yanadhamiria kuleta ushirikiano wa kuleta usalama katika viwango vipya kwa manufaa ya mataifa yote mawili.

Kiongozi huyo wa Somaliland, aliwasili Israel siku ya Jumapili iliyopita kwa ziara yake ya kwanza kabisa ya kiserikali, ambapo Somaliland ilifungua ubalozi mjini Jerusalem.

Ziara hiyo inajiri wiki chache tu baada ya Israel kumteua balozi wake wa kwanza Somaliland, hatua iliyochukuliwa baada ya Somaliland kumteua mjumbe wake nchini Israel.

Mwezi Desemba, Israel ilikuwa nchi ya kwanza kutambua Somaliland kuwa nchi huru, kitendo ambacho kimeukera utawala wa Mogadishu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *