Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imesema viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa ya kufundisha watanzania wakiwemo wakusanya kodi na walipa kodi kwa kuwa wana uwezo wa kufundisha maadili yenye kujenga Imani kwa watanzania hatua ambayo itasaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Kamishna mkuu wa TRA Mcha Hassan Mcha kwa niamba ya kamishna mkuu TRA wakati wa ufunguzi wa kongamano lililowakutanisha viongozi wa Dini na mamlaka hiyo kujadili kuhusu maadili katika ukusanyaji wa mapato wa kodi, ikiwa ni miongoni mwa mambo yatakayofanywa kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya TRA.

Amesema suala la ulipaji wa kodi liko katika vitabu vya Mungu na viongozi hao wanayo nafasi kubwa ya kuwaelemisha waumini wao sawasawa na matakwa ya kisheria na kidini.

Akielezea wajibu huo kidini mwenyekiti Jumuiya ya maridhiano na Amani Tanzania JMAT Sheikh Alhad Mussa Salum amesema watu wasipojengwa kimaadili wataona kama wanadhurumiwa na kuanza kukimbia wajibu wao akawasihi kuona kodi ni jambo la ibada na walifurahie.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *