Mkazi wa Tabata jijini Dar es salaam, Victoria Mkwizu, amejifungua pacha watano wakiwemo wakiume watatu na wa kike wawili.
Victoria amejifungua watoto hao Jumamosi ya juni 13 2026 katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam, watoto wote watano wana afya njema na wanaendelea vizuri.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Hospitali ya taifa Muhimbili imesema jopo la madaktari bingwa wamefanikisha kujifungua salama kwa Victoria ambaye alipewa rufaa ya kwenda hospitalini hapo baada ya kubanika kwa hali yake.
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dkt. Rachel Mhaville amesema tukio hilo ni la kipekee na limehitaji ufuatiliaji wa karibu kutoka kwa timu ya wataalamu wa hospitali hiyo ili kuhakikisha usalama wa mama na watoto.
(Feed generated with FetchRSS)