• Shiru Stuart ashiriki ujumbe wa mafumbo, akiwatia wasiwasi mashabiki kuhusu watoto wa Betty Bayo
  • Madai yaibuka dhidi ya Tash kwa kudaiwa kuficha fedha alizopata Sky kupitia mikataba ya matangazo ya chapa mbalimbali
  • Shiru azitaka kampuni kuwa waangalifu wanaposaini mikataba na watoto wadogo, akisisitiza ustawi wa watoto

Rafiki wa marehemu mwanamuziki wa nyimbo za injili Betty Bayo, Shiru Stuart, ameshiriki ujumbe wa mafumbo uliowaacha mashabiki wengi na wasiwasi.

Betty Bayo (kushoto) akiwa na Shiro Stuart (kushoto na kulia)....
Rafiki wa karibu wa Betty Bayo avunja ukimya wake. Picha: Shiru Stewart.
Source: UGC

Shiru ni msanii na mjasiriamali anayeishi Uingereza ambaye alipata umaarufu kama mmoja wa marafiki wa karibu zaidi wa Betty Bayo baada ya kifo chake.

Akijulikana kama rafiki mkubwa wa Betty Bayo, Shiru alisafiri kutoka Uingereza hadi Kenya kuhudhuria mazishi ya mwimbaji huyo na baadaye akapitia taratibu za kisheria na za usafiri ili kuwapeleka watoto wa marehemu nchini Uingereza kwa likizo ya kukumbukwa pamoja na kuwapa malezi ya muda mrefu.

Mara kwa mara amekuwa akishiriki video za kugusa hisia pamoja na taarifa za watoto hao wakishiriki michezo mbalimbali na kufurahia sikukuu za Krismasi nchini Uingereza, jambo ambalo limekuwa likisifiwa sana na Wakenya kwenye mitandao ya kijamii.

Pia soma

Bintiye Angela Chibalonza Aendeleza Urithi wa Mamake, Aduwaza Watu Kanisani kwa Sauti Tamu

Shiru Stuart alisema nini?

Inaonekana Shiru amemrushia vijembe baba wa kambo wa Sky na Danny kupitia ujumbe wake wa Facebook, jambo lililozua hisia tofauti miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Baada ya baadhi ya wanablogu na Wakenya kumkosoa Hiram Gitau maarufu kama Tash muda mfupi baada ya kifo cha Betty Bayo, mwanamuziki huyo alimtetetea vikali na kumuunga mkono kuwalea watoto wa rafiki yake marehemu.

Hata hivyo, sasa anaonekana kubadilisha msimamo wake na kumkosoa mjane huyo wa marehemu rafiki yake, akidai kuwa amekuwa akizizuia fedha ambazo Sky alipata kupitia mikataba ya matangazo ya chapa mbalimbali.

“Niambieni kwa nini wanawake wawili waliokomaa wanaweza kumuunga mkono mwanaume anayemfukuza mfanyakazi wa nyumbani usiku? Nguvu na akili mnazotumia, kwa nini msijiunge mkono kumsaidia Chiwawa kulipa karo au gharama za usafiri?”

Aliendelea kudai kuwa fedha ambazo Sky alipata kwa kutangaza chapa mbalimbali zilichukuliwa na kwamba alielezwa kuwa atakabidhiwa fedha hizo atakapofikisha umri wa miaka 18.

“Msichana huyo maskini anafanya kazi kwa bidii sana na chapa mbalimbali, lakini fedha hazionekani. Anapoulizia fedha zake, anaambiwa, ‘Nakuekea mpaka ufikishe miaka 18.'”

Pia soma

Magazeti ya Kenya, Juni 14: Macho kwa Ruto huku Wakenya wakitarajia kushuka kwa bei ya mafuta

Shiru alimrushia kijembe Tash na pia kuzionya kampuni za Kenya kuhakikisha zinachukua tahadhari zote muhimu wanaposaini mikataba na watoto wadogo.

“Lakini sote tunajua, ukizaliwa Chiwawa, unabaki kuwa Chiwawa milele. Lakini kula hadi pesa za mtoto? Na hizi chapa za Kenya pia, tafadhali hakikisheni mnachukua tahadhari zote muhimu wakati wa kusaini mikataba na watoto wadogo.”

Katika ujumbe mwingine, aliwauliza wafuasi wake kama wanamfahamu mwanasaikolojia wa watoto au afisa wa ustawi wa jamii mwenye sifa zinazohitajika ambaye anaweza kusaidia watoto walioathiriwa na mazingira ya udanganyifu na ushawishi.

“Natafuta mwanasaikolojia wa watoto au afisa wa ustawi wa jamii nchini Kenya mwenye uzoefu wa kufanya kazi na watoto walioathiriwa na udanganyifu, migogoro ya wazazi au kutengwa na familia.

Watoto hao wamejitenga na watu ambao kwa kweli wana maslahi yao mema moyoni, ikiwemo baadhi ya wanafamilia wa mama yao. Tunaelewa kuwa huenda kumekuwa na ushawishi na udanganyifu mwingi kwa muda mrefu, ndiyo maana tunaona msaada wa kitaalamu unahitajika. (Hata waliambiwa jumba la kifahari ni la kuwatoa kafara).”

Sky anakabiliana vipi na kifo cha mama yake?

Pia soma

Mercy Precious: Pacha wa Mwanafunzi Aliyefariki Utumishi Girls Azungumza kwa Hisia baada ya Mazishi

Katika habari nyingine, Sky alifichua kuwa tangu kifo cha Betty Bayo, amekuwa akijifariji kwa kusikiliza mara kwa mara nyimbo za injili za mama yake.

Mtayarishaji huyo mchanga wa maudhui alikiri kuwa hajui maneno yote ya nyimbo hizo, lakini alisema nyimbo za Kikuyu na Kiswahili sasa zina maana kubwa zaidi kwake.

Sky pia hivi karibuni alikumbuka jinsi Betty Bayo alivyomsukuma kuingia katika ulimwengu wa kucheza dansi na utengenezaji wa maudhui, jambo ambalo sasa analithamini zaidi kuliko hapo awali.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *