Wakielezea hati ya maelewano kati ya Iran na Marekani kuwa ni “kujisalimisha kikamilifu” kwa Iran, wakosoaji wa Donald Trump katika Bunge la marekanii wamesema utawala wake umesalimu amri kwa Jamhuri ya Kiislamu baada ya vita vya gharama kubwa na visivyo na maana ambavyo vilishindwa kufikia malengo yaliyotajwa na Washington.

Mkataba wa hati ya maelewani wenye vifungu 14, uliosainiwa kidijitali na Rais wa Iran Masoud Pezeshkian na Donald Trump jana Jumatano, unatoa wito wa kukomeshwa daima uhasama katika pande zote, ikiwa ni pamoja na Lebanon, kuondolewa vikwazo vya Marekani kwa awamu, kuondolewa mzingiro wa majini dhidi ya Iran ndani ya siku 30, na kurejeshwa usafiri wa kibiashara kupitia Lango-Bahari la Hormuz.

Hati hiyo pia inajumuisha mpango wa ujenzi mpya na maendeleo ya kiuchumi wa Iran kwa ushiriki wa Marekani wenye thamani ya kwa uchache dola bilioni 300, kuruhuusu mauzo ya nje ya mafuta, kuachiliwa mali zinazozuiliwa za Iran, na ahadi mpya ya Iran ya kutotengeneza silaha za nyuklia, huku mazungumzo zaidi yakiendelea kuhusu akiba ya uranium iliyorutubishwa nchini Iran.

Makubaliano hayo yameibua ukosoaji mkali huko Washington, ambapo baadhi ya wabunge wanasema kwamba miezi kadhaa ya mzozo wa kijeshi imesababisha gharama kubwa kwa Marekani na kuifaidisha pakubwa Iran.

Seneta wa Republican Bill Cassidy ameandika kwenye mtandao wa X kwamba: “(Ronald) Reagan anajikunja huko kaburini mwake, miradi ya nyuklia ya Iran yaijaangamizwa, na wamejifunza kwamba kutishia Lango Bahari la Hormuz kunafanya kazi, na bila shaka wataitumia mbinu hii katika siku zijazo.”

Cassidy pia amekosoa vifungu vya kiuchumi vya makubaliano hayo, akisema: “Sasa, Iran itapata nafasi ya kujenga miundombinu mipya kabisa chini ya makubaliano haya.”

Akizungumzia matokeo ya vita, ameongeza kwamba: “Kabla ya vita, Lango-bahari la hormos ulikuwa wazi, Iran ilikuwa ichini ya vikwazo na wanajeshi wetu 13 walikuwa bado hai. Sasa, Wamarekani 13 wameuawa, familia zimelipa mabilioni ya dola za gharama za vita, vikwazo dhidi ya Iran vitaondolewa…”

Kwa upande wake, Seneta wa chama cha Democrat, Chris Murphy ameelezea makubaliano ya Iran na Marekani kuwa “mpango wa kichaa” na “malipo ya mabilioni ya dola bila ya kupata chochote.”

Amekosoa makubaliano hayo kwa kukubali matakwa ya Iran, kama vile kuondolewa vikwazo vya mafuta..

“Makubaliano haya kimsingi ni kwamba tuondoe vikwazo vya mafuta na Iran isifanye loclote mkabala wake… Hiyo ni aibu,” Murphy ameongeza.

Nikki Haley, balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa wakati wa utawala wa kwanza wa Trump, amemshambulia rais wa Marekani kwa “mpango wake wa kuchilia mabilioni ya dola na kuondoa vikwazo dhidi ya Iran, sambamba na ahadi kutoa ya pesa zaidi.”

Mike Pence, ambaye alihudumu kama makamu wa kwanza wa rais wa Trump, pia amesema kwamba Mkataba wa Makubaliano kati ya Marekani na Iran “unafanana na kile kilichokataliwa na utawala wetu katika makubaliano ya nyuklia kati ya Obama na Iran”.

Mwanachama wa Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Seneti, Jeanne Shaheen, ameyataja makubaliano hayo kuwa ni “kujisalimisha kikamilifu” kwa Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *