Baada ya mashabiki, mwamuzi wa Somalia, na kiungo wa Ghana Thomas Partey, suala lingine la visa linalomhusu raia wa Afrika limevuruga Kombe la Dunia la 2026: Elye Wahi wa Côte d’Ivoire karibu aikose mechi dhidi ya Ujerumani nchini Canada, lakini hatimaye ataweza kucheza.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la Soka la Côte d’Ivoire (FIFA) lilitangaza siku ya Alhamisi, Juni 18, kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 hangekuwepo kwa mechi dhidi ya Ujerumani. Alishukiwa kuhusika katika kamari ya michezo iliyojaa udanganyifu nchini Ufaransa kufuatia kadi ya njano aliyopewa wakati wa mechi iliyopita ya Ligue 1 na klabu yake, OGC Nice. Côte d’Ivoire wanatarajiwa kumenyana na Ujerumani siku ya Jumamosi, Juni 20, huko Toronto kwa mechi yao ya pili ya Kundi E katika michuano ya Kombe la Dunia la 2026.

Kwa hivyo kesi yake ni tofauti na ile ya Thomas Partey wa Ghana, mchezaji wa kwanza wa Kombe la Dunia aliyekataliwa kuingiaCanada: kiungo huyo kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya ubakaji nchini Uingereza. Serikali ya Ghana ilipambana katika mahakama ya Canada ili uamuzi wa kunmyima visa mchezaji huyo ubatilishwe, bila mafanikio. Kwa hivyo, Black Stars ilicheza bila mchezaji huyo wa Villarreal katika ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Panama siku ya Jumatano, Juni 17, huko Toronto.

Marekani, kwa upande wake, ilikataa kutoa visa kwa wajumbe wa mashabiki – haswa kutoka Côte d’Ivoire na Senegal – na ikamfukuza mwamuzi wa Somalia Omar Artan, licha ya kuwa na visa halali, ikidai “anahusishwa na watu wanaoshukiwa kutoa makundi ya kigaidi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *