
NAIROBI – Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limeanzisha kampeni ya haki kutekelezwa kwa waathiriwa wa vita mashariki wa DRC.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kampeini hiyo iliopewa jina “6 million Voices for Justice for Congo, inalenga watu millioni sita duniani kusaini ombi la kuwafidia waathiriwa wa vita mashariki mwa DRC.
Amnesty International inataka kuanzishwa kwa chombo cha kimataifa cha mahakama kitakachochunguza uhalifu uliotekelezwa kati ya mwaka 1993 na 2003 na makudni yaliojihami nchini DRC, Shirika hilo linasema mapigano hayo yamesababisha madhara makubwa kwa raia.
Naibu mkurugenzi wa Amnesty International kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Vongai Chikwanda, amesema waathiriwa wa Congo wameahidiwa haki kwa miongo kadhaa bila wahusika wengi kuwajibishwa.
Aidha, Amnesty International inapendekeza tarehe mosi Oktoba iwe siku ya kitaifa ya tafakari na hatua dhidi ya uhalifu wa kivita nchini DRC, ikiwa ni kumbukumbu ya ripoti ya umoja wa mataifa ya mwaka 2010 iliyobaini ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, huku mapendekezo mengi ya ripoti hiyo yakiendelea kupuuzwa