
NAIROBI – Mataifa ya Ulaya, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani yameeleza wasiwasi wao kuhusu vitendo vinavyotekelezwa na wapiganaji wa RSF katika mji wa Al Obeid, nchini Sudan, mataifa hayo yakisema matokeo yake yanaweza kuwa uhalifu wa kivita.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mataifa hayo, ambayo yamewasilisha malalamishi yao kwa baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa, yamesema vita vinavyoendelea katika mji huo wa Al Obeid vinahatarisha maisha ya raia zaidi ya nusu milioni, na kutaka RSF kusitisha mara moja operesheni zake katika mji huo.
Mataifa hayo pia yametaka jamii ya kimataifa kushinikiza pande hasimu nchini Sudan kusitisha vita ili kuzuia athari za mapigano yanayoendelea kuwakumba raia.
Mji wa Al Obeid ni mojawapo ya miji mikubwa katika jimbo la Kordofan Kaskazini nchini Sudan, na katika siku za karibuni umeshuhudia mapigano makali kutoka kwa waasi wa RSF wanaolenga kuudhibiti.