Marekani imetangaza siku ya Alhamisi kwamba inaweka vikwazo kwa maafisa wa Tigray People’s Liberation Front (TPLF), wanaoshutumiwa kudhoofisha amani nchini Ethiopia.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inabainisha kwamba kuongezeka kwa mvutano kati ya wanamgambo wa TPLF na serikali ya shirikisho kunatishia kufufua mgogoro katika eneo la Tigray.

Majina ya wale waliolengwa hayajatolewa. Vikwazo hivyo vinaweka vikwazo vya visa kwa maafisa na wanafamilia wao.

TPLF na mamlaka huko Addis Ababa wanashutumuina kwa kutaka kuanzisha tena uhasama. Vikosi vya kikanda huko Tigray vilizindua shambulio baya dhidi ya wanajeshi wa shirikisho mnamo mwezi Novemba 2020.

Mapigano yalimalizika kwa makubaliano ya amani mnamo mwaka 2022. Hata hivyo, makubaliano haya yamekuwa dhaifu zaidi tangu mwaka uliopita.

Ingawa ilipigwa marufuku kufanya shughuli zozote za kisiasa, TPLF ilifanya uchaguzi wa magavana mnamo mwezi Mei, na hivyo kukiuka kifungu muhimu cha makubaliano ya amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *