Timu ya taifa ya Mexico imekuwa ya kwanza kufuzu hatua inayofuata ya mashindano baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Korea Kusini.
Mexico, ambayo ilishinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Afrika Kusini kwa mabao 2 kwa baada ya sherehe za ufunguzi jijini Mexico City, ilipata ushindi wake wa pili Alhamisi usiku baada ya Romo kufunga bao pekee la mchezo katika dakika ya 50.
Kwa ushindi huo, Mexico imefikisha pointi sita na kufuzu rasmi hatua inayofuata huku ikiwa bado haijaruhusu kufungwa bao lolote katika mashindano hayo.
Korea Kusini, ambayo ilifanya mgeuko wa kuvutia na kuifunga Czechia katika mchezo wake wa kwanza, ilikuwa ikitarajia kufuzu kwa kuishinda Mexico
Hata hivyo, baada ya kipigo hicho, italazimika kuepuka angalau kushindwa katika mechi yake ya mwisho dhidi ya Afrika Kusini ili kuendelea na mashindano.

(Feed generated with FetchRSS)