#HABARI: Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani limeanza kusikiliza shauri namba 47 la mwaka 2026, lililofunguliwa na wananchi 147 wanaopinga kubomolewa kwa makazi yao katika shamba lenye hati namba 94628 lililopo Changwahela, Kata ya Mapinga.
Wananchi hao wanapinga utekelezaji wa hukumu ya kesi ya mwanzo ya mwaka 2019 iliyompa ushindi Bwana James Mpayo, wakidai kuwa wao hawakushirikishwa wala kuwa sehemu ya washtakiwa wanane waliolamikiwa tangu awali.
Mzozo huo unahusisha eneo lenye ukubwa wa takribani hekari 34, ambapo wananchi hao wanadai kuwa watu wanane walioshtakiwa hapo awali na kupoteza rufaa yao mwaka 2025, hawakuwa wakazi halisi wa eneo hilo.
Hatua ya Bwana Mpayo kuanza taratibu za utekelezaji wa amri ya Mahakama ya kuwaondoa wananchi hao baada ya yeye kushinda kesi, ndiyo iliyozua taharuki na kuwalazimu wakazi hao kukimbilia barazani kuomba kuzuia ubomoaji huo.
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Rajabu Mnyukwa, ameahirisha shauri hilo hadi Julai 1, 2026, ili kumpa fursa mlalamikiwa wa kwanza, James Mpayo, kuwasilisha majibu yake ya maandishi.
Pande zote mbili, zikiwemo Wakili Walter Godluck anayewakilisha wananchi na mawakili wa upande wa utetezi, ziliridhia ucheleweshaji huo ambao pia utatumika kutoa hati mpya za wito kwa wajibu maombi wengine wanane walioshindwa kufika mahakamani leo.
Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
Capitalradio Tanzania
(Feed generated with FetchRSS)