Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na madini yote kama vitamini na protini.
Mama mjamzito anatakiwa apate gramu 100 za protini kila siku.

Source: Getty Images
Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa afya bora.
TUKO.co.ke iliweza kukundalia vyakula 10 bora ambavyo mama mjamzito na mtoto wake wanastahili kula
1. Jamii Kunde
Mbegu za makundekunde ni sehemu muhimu ya chakula kwa mama mjamzito kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha protini.
Kwa watu wasiokula nyama au wana uwezo mdogo tu kujipatia nyama mbegu za jamii kunde zinatosheleza mahitaji ya protini.
Hivi ni vyakula vya mimea kama Soya,Peas,Karanga, Alfa alfa,Mikunde, maharage.
2. Mayai
Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protini, vitamini A na madini ambayo itasaidia kuzuia kupatwa na maradhi ya magonjwa mbali mbali.
3. Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa
Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi na siagi.

Pia soma
Mwigizaji wa Mother-In-Law Maria asimulia sababu ya ndoa yake kukatika: “Nimekuwa singo miaka 15”
Maziwa ni muhimu kwa protini, calcium, vitamini na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa na misuli,
Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi na kusawazisha mdundo wa moyo.
4. Viazi tamu
Viazi vitamu vina vitamini A ambayo husaidia ukuaji wa macho ya mtoto,ngozi na mifupa
5. Nyama
Nyama ya nguruwe,kuku au ngombe huwa na protini mingi sana na husaidia katika ukuaji wa mwili wa mtoto hasa kwa mama mjamzito wa miezi minne
6. Nafaka na vyakula vya Wanga
Vyakula hivi huipa mwili nguvu ya kufanya kazi na pia ukuaji wa mtoto tumboni.Vyakula hivi ni kama mahindi,mtama ,mihogo,vyakula vya ngano kama mkate n.k.
7. Avocado
Ni matunda ambayo yana mafuta mengi maarufu kama fatty acid.
Avocado inasaidia katika ukuaji wa ubongo,ngozi nyororo na ukuaji wa misuli ya mtoto tumboni.
8. Mboga za majani
Mboga za majani kama spinach, kabeji, mchicha na matembele. Mboga hizi zinafaa ziwe zenye rangi ya kijani iliyokolea kwa sababu hizi ndizo zenye virutubisho vya kutosha.
Mboga hizi zitampa mama na mtoto wake Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kupata protini ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu.

Pia soma
Kombe la Dunia 2026: Mshahara wa Rais wa FIFA Gianni Infantino baada ya nyongeza kubwa ya bonasi
Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata ugonjwa wa Anemia.
9. Mafuta ya samaki
Mafuta ya maini ya samaki huwa na Omega fatty acids ambayo inasaidia ukuaji wa ubongo na macho ya mtoto.
10. Maji
Maji ni muhimu kwa mwili kwa sababu inasaidia kwenye mmenyenyo na unyonywaji chakula na pia husaidia kuzia choo ngumu
Maji pia huzuia uvimbe wa mwili na maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI)
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke