Jumatatu, Juni 22, magazeti ya kitaifa yaliripoti kwa mapana kuhusu maandamano ya ukumbusho yaliyopangwa kufanyika Juni 25.

Magazetini
Magazetini: Mvutano wa NPSC na Wakuu wa Polisi Watikisa Huduma ya Polisi Nchini
Source: UGC

Magazeti mengine pia yaliripoti kuhusu mvutano wa madaraka kati ya makamishna wa kiraia wa Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi (NPSC) na wakuu wa polisi.

1. Daily Nation

Vita vya muda mrefu vya ubabe wa mamlaka kati ya makamishna wa kiraia wa Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi (NPSC) na wakuu wa polisi wakiongozwa na Inspekta Jenerali Douglas Kanja vimesimamisha majukumu muhimu ya usimamizi wa rasilimali watu, hali ambayo imeathiri pakubwa ari ya kazi ndani ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS).

NPSC, ambayo imepewa jukumu la kusimamia rasilimali watu kwa Polisi wa Kenya, Polisi wa Utawala na Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai (DCI), haijafanya kikao chochote tangu Oktoba mwaka jana kutokana na mgogoro huo ambao bado haujapatiwa suluhu.

Mvutano huo ulizidi baada ya zoezi lenye utata la kuajiri maafisa 10,000 mwezi Oktoba, ambapo wakuu wa polisi walipuuza miongozo ya NPSC wakidai kuwa kulikuwa na njama za kunyakua mamlaka ya Inspekta Jenerali.

Pia soma

Mbunge Alfred Mutai asakwa baada ya kufyatua risasi na kujeruhi kadha katika hafla ya Susan Kihika

Mzozo huo uliishia mahakamani na kusababisha Mahakama ya Rufaa kutoa uamuzi mnamo Februari 27 uliosimamisha hukumu ya mahakama ya chini iliyokuwa imempa Inspekta Jenerali mamlaka ya kipekee ya kupandisha vyeo na kufukuza kazi maafisa wa polisi.

Wakati jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa Daniel Musinga, Mumbi Ngugi na George Odunga liliruhusu mafunzo ya maafisa walioajiriwa kuendelea, pia lilisitisha kupandishwa vyeo na kufutwa kazi kwa maafisa wote wa polisi hadi rufaa kuu itakaposikilizwa na kuamuliwa ili kuepusha “madhara yasiyoweza kurekebishwa.”

Kutokuridhika kunakoendelea kumezua taharuki miongoni mwa viongozi wa juu kuhusu uwezekano wa kuvurugika kwa maandalizi ya usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Katika juhudi za kutafuta suluhu, Naibu Rais Kithure Kindiki aliitisha kikao cha siri kilichodumu kwa saa tano katika makazi yake ya Karen.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen, Inspekta Jenerali Kanja, Mkurugenzi wa DCI Amin Mohamed pamoja na makamishna wa kiraia wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Profesa Collette Suda.

Lengo la mkutano huo lilikuwa kufikia mwafaka wa kusitisha mzozo huo, lakini juhudi za kuwashawishi makamishna kuondoa kesi iliyoko Mahakama ya Rufaa ziligonga mwamba bila kufikiwa kwa makubaliano yoyote.

Pia soma

Ruto Amrushia Gachagua Makombora Mazito Katika Hotuba Moto: “Inaonekana Hunijui”

2. The Standard

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat amewahakikishia wananchi kuwa hatua za kina za usalama zimewekwa kote nchini kuelekea maandamano ya ukumbusho yatakayofanyika Juni 25.

Maandamano hayo yamepangwa kuwakumbuka waathiriwa waliopoteza maisha wakati wa maandamano ya kupinga serikali mwaka 2024 na 2025.

Lagat alizungumza mjini Mombasa wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuwawezesha kiuchumi vijana 25 kutoka familia zenye kipato cha chini.

Alisisitiza kuwa ingawa polisi wataheshimu haki ya kikatiba ya wananchi kufanya maandamano ya amani, watakuwa na msimamo mkali dhidi ya vitendo vya uvunjaji wa sheria.

Mkuu huyo wa polisi alieleza kuwa vyombo vya usalama havina mpango wa kuwazuia wananchi wanaofanya maandamano kwa amani, lakini akaonya kuwa maandamano yakigeuka kuwa vurugu au uharibifu wa mali, hatua za haraka za utekelezaji wa sheria zitachukuliwa.

“Hatuna tatizo lolote. Wakenya wataendelea na shughuli zao za kila siku. Wale watakaosababisha vurugu watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Nataka kusema kuwa Wakenya wako huru kuendelea na kazi zao. Tutatoa usalama kwa Wakenya wote na wale watakaosababisha fujo watakamatwa,” Lagat alisema Jumamosi, Juni 20.

Pia soma

NEC ya ODM Haikufuata sheria katika kumdondosha Edwin Sifuna, mahakama ya mizozo ya kisiasa yasema

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *