Tume ya uchaguzi nchini Sudan Kusini, imetangaza kwamba uchaguzi wa urais utaandaliwa Disemba 22 mwaka huu wa 2026, baada ya zoezi hilo lililosubiriwa kwa hamu kuahirishwa mara kadhaa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ni tangazo linalotolewa licha ya hali mbaya ya usalama huku waangalizi wa kimataifa wakionya juu ya taifa hilo la Afrika mashariki kurejea kwenye vita vya wenywe kwa wenyewe kutokana na mzozo unaozidi kuongezeka kati ya vikosi vya serikali na vya upinzani.

Mkataba wa amani wa 2018 uliomaliza vita kati ya rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Riek Machar, kwa kiasi kikubwa umeonekana kutotekelezwa, na kuliacha taifa hilo kwenye hali mbaya ya umasikini pamoja na viwango vya juu vya ufisadi.

Chini ya mchakato wa amani, uchaguzi mkuu ulitakiwa kuandaliwa mwaka wa 2022, lakini ukacheleweshwa hadi 2024 na baadaye kuahirishwa tena hadi mwaka huu.

Licha ya kutoa tangazo hilo, mwenyeketi wa tume ya uchaguzi Abednego Akok Kacuol, ameonya kuwa bado kuna sintofahamu kwenye masharti kadhaa ya mkataba wa amani yanayotakiwa kuruhusu uchaguzi huo kufanyika.

Kulingana na Akok, kwa sasa tume hiyo imepokea dola milioni 21 kati ya dola milioni 250 zilizopendekezwa kwa ajili ya shughuli hiyo, huku pia akitaja suala la usalama kusalia changamoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *