Moto katika jengo linalohifadhi maktaba na kituo cha kufundishia wanafunzi uliwaua watu wasiopungua 14 nchini India siku ya Jumatatu, mamlaka zimesema.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Moto huo ulizuka Lucknow, mji mkuu wa jimbo la Uttar Pradesh kaskazini mwa India, kwenye ghorofa ya kati ya jengo la kibiashara la ghorofa tatu katika eneo la makazi, kabla ya kuenea haraka hadi ghorofa ya juu.

“Watoto kumi na wanne waliangamia katika tukio hili,” naibu waziri mkuu wa jimbo hilo, Brajesh Pathak, amewaambia waandishi wa habari, akiongeza kuwa watu wengine wanne walijeruhiwa katika kisa hicho cha moto.

Haijabainika wazi kama waathiriwa wote walikuwa wanafunzi.

Wanafunzi kadhaa waliruka kutoka ghorofa ya juu ya jengo hilo kwa kuepuka moto, mashahidi wamemwambia mwandishi wa habari wa AFP.

Televisheni ya India imerusha picha za moto ukitoka kwenye sehemu ya mbele ya jengo hilo huku wazima moto wakijitahidi kudhibiti moto huo.

Jengo hilo lilikuwa na kituo cha usaidizi wa wanafunzi na maktaba.

Visa vya moto kwenye majengo ni jambo la kawaida nchini India kutokana na ukosefu wa vifaa vya kuzima moto na kupuuzwa kwa kanuni za usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *