Rais wa Iran Masoud Pezeshkian anatarajiwa kuzuru Pakistan kufanya mazungumzo na maofisa ambao wamekuwa kwenye mazungumzo ya upatanishi kati ya Tehran na Washington.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ziara yake ni ya kwanza nchini Pakistan tangu Marekani na Israeli kuishambulia Iran Februari 28, na inajiri wakati huu timu za kiufundi zikifanyia kazi makubaliano kati ya Iran na Marekani.
Pakistan ilikuwa mpatanishi mkuu kwenye mazungumzo yasiokuwa ya moja kwa moja kati ya Marekani na Iran kabla ya makubaliano ya agenda 14 yaliotiwa saini wiki iliopita.
Usalama umeimarishwa mjini Islamabad ambapo Rais wa Iran anatarajiwa kukutana na Rais Asif Ali Zardari na Waziri Mkuu Shehbaz Sharif.
Pezeshkian na Sharif wanatarajiwa kuwa na mazungumzo na baadaye kuzungumza na wanahabari kuhusu walichokizungumzia.