Dar es Salaam. Jamhuri katika kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara, Rehema Hassan (42), imeieleza Mahakama bado wanaendelea na uchunguzi.

Kwa sababu hiyo, Rehema ambaye ni mkazi wa Kigamboni Mwapemba, jijini Dar es Salaam ataendelea kusalia mahabusu hadi Juni 6, 2026 itakapotajwa kesi hiyo kwa njia ya mtandao.

Hatua hiyo inatokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokukamilika.

Rehema anadaiwa kumuua muongozaji na Msimamizi wa sauti za filamu nchini, Athuman Nyanza.

Leo Jumanne, Juni 23, 2026 Wakili wa Serikali, Erick Mabagala ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi hiyo ilipotajwa kwa njia ya video huku mshtakiwa akiwa mahabusu.

Alidai Rehema hajaletwa Mahakamani hapa na wapelelezi bado unaendelea uchunguzi, hivyo aliomba mahakama iwapangie tarehe nyingine

Mbagala ametoa taarifa hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga, anayesikiliza kesi hiyo.

Hakimu Mwankuga, alikubaliana na ombi la upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 6, 2026 kwa kutakwa.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Rehema anadaiwa Februari 10, 2026 eneo la Mwapemba lililopo Kigamboni mkoa wa Dar es Salaam,  ulimuua Athuman Nyanza.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo, kinyume na kifungu kifungu196 na kifungu 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2023.

Kwa mara ya kwanza, mshtakiwa alifikishwa Mahakamani hapo Aprili 29, 2026 na kusomewa shtaka hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *