
Utawala wa kijeshi wa Niger, umewasilisha rasmi barua ya kutaka kujitoa kama mwanachama wa mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita, hatua hii ikija miezi tisa kupita tangu itangaze kuwa itafanya hivyo sambamba na Mali pamoja na Burkina Faso.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Nchi hizi tatu za ukanda wa Saheli zote zinatawaliwa na serikali za kijeshi zenye msimamo mkali na ambazo ziliingia madarakani kwa mapinduzi mwaka 2020 na 2023 na zimewageuzia kisogo nchi za Magharibi.
Mataifa haya yalitangaza kwa pamoja kujiondoa katika mahakama ya ICC mwezi Septemba mwaka jana, wakiita mahakama hiyo “chombo cha ukandamizaji na ukoloni mamboleo chini ya ubeberu”.
Mahakama ya ICC imethibitisha kupokea barua ya nchi ya Niger inayoongozwa na jenerali Abdourahamane Tiani, Juni 18, na mchakato wake utakamilika kufikia Juni 18, 2027, hata hivyo katika kipindi hiki Niger lazima iheshimu majukumu yake kwa mahakama hiyo hadi tarehe hiyo itakapofika.
Kwa sasa mahakama ya ICC ina nchi wanachama 125, huku Marekani, Urusi, Israeli, China na Myanmar zikiwa miongoni mwa mataifa ambayo si wanachama wa mahakama hiyo.