
Ripoti mpya ya umoja wa Mataifa, imeonesha kuwa unyanyasaji wa kingono unazidi kutumika kama “silaha ya vita” nchini Sudan ili kuwatisha raia.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwenye ripoti yake, Ofisi ya haki za bindamu ya Umoja wa Mataifa imethibitisha visa 546 vya dhuluma za kimapenzi ikiwemo ubakaji na utumwa kwa kingono tangu kuzuka kwa vita kwenye taofa hilo miaka mitatu iliopita.
Aidha karibu watu 838 waliripotiwa kudhulumiwa wakiwemo wanawake 539, wasichana 284, wanaume wanane na vijana wakiume saba.
Katika hatua nyengine, Uingereza na mataifa mengine sita ya Ulaya yametoa wito wa kusitishwa kwa vurugu katika Mji wa el-Obeid, ambao unaripotiwa kuzingirwa na wapiganaji wa RSF na washirika wake.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Yvette Cooper amesema RSF inatumia ndege nyuki (droni) kushambulia miundombinu ya kiraia pamoja na kuwazuia raia kutoka kwenye Mji wa el-Obeid kupata mahitaji muhimu, ambapo zaidi ya watu laki tano wanaishi katika Mji huo.