Kikosi cha Wanamaji la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimeshambulia ngome za kijeshi za Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia kulipiza kisasi uchokozi wa awali dhidi ya maeneo ya pwani ya Iran.

Kikosi hicho kimesema hayo katika taarifa iliyotolewa jana Ijumaa, kikisema kwamba kisasi hicho “kimelenga maeneo ya jeshi la kigaidi la Marekani Magharibi mwa Asia.”

Taarifa hiyo imesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya vikosi vya jeshi la Marekani kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya pwani ya Iran kama sehemu ya “mfumo usiobadilika wa Marekani wa kukiuka majukumu yake.”

“Katika kufanya uchokozi huo, Washington imetumia “visingizio mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupita meli isiyofuata sheria katika njia ambayo haikuidhinishwa katika Lango-Bahari la Hormuz,” imeongeza taarifa hiyo.

Hapo awali, Kamandi Kuu ya Majeshi ya Marekani ilikuwa imeripoti kuwa imefanya mashambulizi dhidi ya baadhi ya malengo nchini Iran.

Wanajeshi wa Marekani waliotumwa katika eneo la Asia Magharibi walidai kuwa walifanya uchokozi huo badala ya kile walichokielezea kama, shambulio la Alhamisi la ndege zisizo na rubani dhidi ya meli, ambayo waliipa jina la meli ya mizigo ya MV Ever Lovely yenye bendera ya Singapore. Limedai kwamba shambulio hilo lilitokea wakati meli hiyo ilipokuwa ikiondoka kwenye Lango-Bahari la Hormuz kando ya pwani ya Omani.

Jamhuri ya Kiislamu, imekuwa iikikanusha madai ya kulenga vifaa visivyo vya kijeshi, na kuonya kuhusu jitihada za kuihusisha na mashambulizi kama hayo kwa kuanzisha shughuli zinazofanyika chini ya “bendera ya uongo”.

Jeshi la Wanamaji la IRGC pia limeeleza kwamba Marekani ilitaka kukiuka majukuumu yake chini ya mkataba wa maelewano uliosainiwa hivi karibuni kati ya pande hizo mbili “kupitia vitendo vya uchochezi wa aina mbalimbali.”

“Na sasa imepokea jibu linalohitajika,” taarifa hiyo imeendelea kusema, ikimaanisha kulipiza kisasi kwa jeshi hilo. “Hilo litatumika pia kwa ukiukwaji wowote wa baadaye wa makubaliiano hayo,” imeongeza taarifa ya IRGC.

“Ikiwa uchokozi huo utarudiwa, majibu yetu yatakuwa mapana zaidi kuliko haya,” imesisitiza taarifa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *