Nchini Venezuela idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na matetemeko mawili ya ardhi yaliyotokea wiki hii jijini Caracas, imefikia karibu  Elfu Moja, wakati huu waokoaji wa Kimataifa wakiendelea kutawafuta watu waliofukiwa kwenye vifusi vya majengo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais wa mpito Delcy Rodriguez amesema, bado ana matumaini makubwa ya kupatikana hai kwa manusura wa janga hilo lilitokea siku ya Jumatano.

Kwa siku ya tatu, hivi leo, waokoaji wa kimataifa wameendelea kuwatafuta watu ambao hawajaonekana, wakati huu idadi ya vifo ikifika 920 wakiwemo raia 28 wa Ureno, huku wengine zaidi ya 3,300 wakijeruhiwa.

Rais wa mpito Delcy Rodriguez amesema, bado ana matumaini makubwa ya kupatikana hai kwa manusura wa janga hilo lilitokea siku ya Jumatano.
Rais wa mpito Delcy Rodriguez amesema, bado ana matumaini makubwa ya kupatikana hai kwa manusura wa janga hilo lilitokea siku ya Jumatano. © Fernando Vergara / AP Photo

Tom Fletcher, Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia misaada ya kibinadamu amesema, watoa misaada zaidi ya 2,000 wapo nchini Venezuela wanakoendelea kutoa misaada hasa kuwatafuta watu zaidi ya 50,000 ambao mpaka sasa hawajapatikana.

Kwa wale walionusirika, wanakabiliwa na changamoto nyingine ya kukosa makaazi na chakula, baada ya nyumba zao kuporomoka. Kwa sasa wamelazimika, kukimbilia katika makambi ya muda mfupi na shule wanakoishi kwa sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *