
Wakulima 17 wameuawa Kaskazini Magharibi mwa nchi ya Nigeria, baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kiongozi wa kisiasa katika wilaya ya Talata Mafara, Yahaya Abubakar Yari, amesema watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki waliwavamia wakulima hao walipokuwa katika makaazi yao katika Kijiji cha Tungar Baure jimboni Zamfara.
Mbali na mauaji, watu hao wenye silha wamewateka idadi ya watu isiyojulikana wakati huu wakaazi wa eneo hilo wakiendelea kulalamikia utovu wa usalama.
Juni tarehe 12, watu wengine wenye silaha, waliwauwa wakulima 12 na kuwaacha wengine watano na majeraha, walipokuwa wanaendelea na shughuli zao mashambani katika Kijiji jirani katika wilaya ya Maradun.
Shambulizi hili limetokea anakotokea Naibu Waziri wa Ulinzi Bello Muhammad Matawalle, ambaye amewahi kuahidi kutuma wanajeshi 2,000 katika eneo hilo ili kuwakabili watu wenye silaha.