Siku moja baada ya Serikali kulielekeza Jeshi la Polisi nchini kusitisha utoaji wa vibali kwa vyama vya siasa kwa ajili ya mikutano ya hadhara na mikusanyiko mbalimbali, Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) imesitisha maadhimisho ya Wiki ya Wazazi yaliyokuwa yafanyike jijini Mwanza kuanzia Juni 30 hadi Julai 4 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Fadhili Maganya, amesema uamuzi huo umefikiwa kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Serikali pamoja na maslahi mapana ya kulinda amani na usalama wa wananchi, huku akibainisha kuwa tarehe mpya za maadhimisho hayo zitatangazwa baadaye baada ya mazingira kuruhusu kufanyika kwa shughuli hizo.

✍🏾✍🏾 @amaniel_mmbando

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *