Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), leo Juni 27, 2026 imefanya mbio na Matembezi ya Shukrani kwa Mlipakodi katika mikoa yote nchini ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuelekea uyoaji wa Tuzo ya Rais kwa Mlipakodi Bora na Maadhimisho ya Miaka 30 ya TRA yatakayofanyika Julai Mosi, 2026.

Katika Mkoa wa Dar es Salaam, mbio hizo zimefanyika katika Viwanja vya Gymkhana na kuhudhuriwa na watumishi wa TRA, wadau, wafanyabiashara na walipakodi na kuongozwa na Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omary.

Mbio na matembezi hayo yamefanyika kwa lengo la kutoa shukrani kwa walipakodi kwa mchango wao mkubwa katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali na maendeleo ya Taifa, sambamba na kuhamasisha ushiriki wa wadau katika Maadhimisho ya Miaka 30 ya TRA na hafla ya Tuzo ya Rais kwa Mlipakodi Bora.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *