• Rais William Ruto alimtetea naibu wake Kithure Kindiki huku kukiwa na tetesi kuhusu mustakabali wa safari yake ya kisiasa kuelekea uongozi wa juu
  • Rais aliahidi kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo, ikiwemo uboreshaji wa miundombinu na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu
  • Kindiki alieleza miradi ya serikali inayowanufaisha wakazi wa Kaunti ya Meru huku akipuuzilia mbali ushawishi wa viongozi wa upinzani

Nancy Odindo ni mwandishi wa masuala ya sasa katika TUKO.co.ke (alijiunga mwaka 2023). Ana uzoefu wa mwaka mmoja katika vyombo vya habari vya kuchapisha na zaidi ya miaka mitano katika vyombo vya habari vya kidijitali.

Rais William Ruto amedokeza anamuunga mkono naibu wake Kithure Kindiki.
Rais William Ruto anasema naibu wake Kithure Kindiki anafaa kuwania urais. Picha: Kithure Kindiki.
Source: Facebook

Rais William Ruto amedokeza kuwa atamuunga mkono naibu wake Kithure Kindiki kupanda ngazi hadi urais baada ya kumaliza muhula wake.

Ruto alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake katika Kaunti ya Meru mnamo Jumapili, Juni 28, huku kukiwa na tetesi kwamba Kindiki anaweza kutengwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Je, Ruto atamuunga mkono Kithure Kindiki kuwania urais?

Pia soma

Magazetini Jumatatu, Juni 29: Ripoti ya Siri kwa Ruto Yafichua Mzozo wa Kanja na NPSC

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa mabadiliko ya kisiasa katika eneo la Mlima Kenya yanaweza kuathiri nafasi ya Ruto kuchaguliwa tena, jambo ambalo limezua maswali kuhusu mustakabali wake na naibu rais wa sasa.

Akizungumza na wakazi wa Maili Tatu, rais aliwapuuza wakosoaji wake pamoja na wanaompinga Kindiki, akisema kuwa Kindiki anafaa kwa jukumu hilo na kuwaonya wanaomdharau kuwa watashangazwa.

Kihistoria, iwapo Ruto atashinda uchaguzi ujao na kuhudumu mihula yake, Kindiki anaweza kuwania urais mwaka 2032.

“Je, hafai? Kuna watu wanaojaribu kumdharau na kumshusha hadhi. Nataka kuwaambia watashangaa wakati wake utakapofika. Huyu jamaa anafaa kwa kazi hiyo. Ukimlinganisha na yule mwingine ambaye amejaa ukabila, chuki na fitina, huyu profesa anaelewa mambo vizuri zaidi. Mwacheni aendelee kufanya kazi,” alisema Ruto.

Aidha, mkuu huyo wa nchi aliendelea kuwashambulia viongozi wa upinzani, akiwahakikishia kuwa watashindwa mapema katika uchaguzi wa 2027.

Pia aliangazia miradi ya maendeleo na mipango ya serikali kwa wakazi wa Meru, ikiwemo ujenzi wa Daraja la Nithi, sekta ya elimu, nyumba za gharama nafuu na miradi mingine ya miundombinu.

Ruto alizindua miradi gani Meru?

Katika hotuba yake, Kindiki alimpongeza Ruto na kuwasihi wakazi wa Meru kuendelea kumuunga mkono huku akiwapuuza viongozi wa upinzani wanaojaribu kuwashawishi.

Pia soma

Kanyari apiga abautani, akubali kushirikiana na Tash kuwalea watoto lakini kwa masharti mazito

Rais William Ruto alikuwa amezungumza na wakaazi wa Meru katika ziara ya maendeleo.
Rais William Ruto amtetea naibu wake Kithure Kindiki kabla ya uchaguzi wa 2027. Picha: William Ruto.
Source: Facebook

“Rais amekuja hapa kwa sababu anatuletea uwanja wa michezo Maua, Soko la Kangeta na miradi mingine. Hajaja kufanya siasa. Kama jamii ya Meru, hatutakubali mtu yeyote atudharau au atuambie tuondoke serikalini tukaanzishe nyingine. Huo ni upuuzi. Kwa nini wanataka tutoke serikalini? Ninaunga mkono Ruto atafute muhula wa pili ili akamilishe dhamira ya Tutam,” alisema.

Alisema serikali inaiboresha Hospitali ya Meru kutoka kiwango cha Level 5 hadi Level 6 kwa gharama ya KSh bilioni 1.

Aidha, KSh bilioni 20 zinatumika kujenga nyumba za gharama nafuu na mabweni ya wanafunzi, KSh bilioni 8 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya barabara, huku KSh bilioni 7 zaidi zikielekezwa katika ujenzi wa Daraja la Nithi.

“Kaya 27,000 zaidi katika Kaunti ya Meru zinaunganishwa na umeme kwa gharama ya KSh bilioni 2.3, huku ujenzi wa Uwanja wa Maua wenye thamani ya KSh milioni 250 ukianza wiki hii,” alisema Kindiki.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *