g

Chanzo cha picha, Bloomberg via Getty Images

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza mazungumzo mapya kati ya wawakilishi wa Marekani na Iran mjini Doha, akisema kuwa mazungumzo hayo “yanaweza kuwa muhimu”.

Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekanusha kuwepo kwa mpango wowote wa mazungumzo katika siku za karibu, ikisema safari ya wawakilishi wake kwenda Doha inalenga kufuatilia kuachiwa kwa mali za Iran zilizogandishwa.

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema dola bilioni sita kati ya dola bilioni 12 za mali za Iran zilizogandishwa zitaachiliwa na hivi karibuni zitapatikana kwa serikali.

Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imejibu kauli za Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa kusisitiza kwamba shughuli za kuondoa mabomu ya baharini katika Mlango wa Hormuz zitafanywa na Iran pekee.

Maelezo zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *