Nchini Senegal, wabunge 129 kati ya 129 walioshiriki kikao cha Bunge wamepiga kura ya kuunga mkono mageuzi ya katiba mnamo Juni 29, 2026, huko Dakar, mwishoni mwa kikao chenye ghasia kilichojaa maandamano nje ya Bunge, kufukuzwa kwa mwanachama wa chama cha Alliance for the Republic (APR) cha rais wa zamani Macky Sall ambaye alikataa kutoka jukwaani, na wanachama wa upinzani kususia kura.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Dakar, Juliette Dubois

Waziri wa Sheria alitangaza katika juma la mikutano la Bunge kwamba mageuzi haya yatawasilishwa kwa kura ya maoni.

Nchini Senegal, wabunge walipiga kura kuhusu mageuzi ya katiba siku ya Jumatatu Juni 29, 2026, huko Dakar chini ya mvutano mkali. Mageuzi hayo yatawasilishwa kwa kura ya maoni, Waziri wa Sheria alionya. Hata kabla ya kikao kuanza saa 4:00 asubuhi, vikosi vya usalama vilitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa Alliance for the Republic (APR) – chama cha rais wa zamani Macky Sall – na makundi mengine ya upinzani waliokuwa wakiandamana karibu na Bunge. Watu walikamatwa, na kisha njia ya kuingia kwenye jengo hilo ilizuiwa.

Mvutano huo ulienea ndani ya chumba mikutano ya Bunge. Mbunge wa chama cha APR Abdou Mbow alikataa kutoka jukwaani, akidai mihjadala isitishwe. Wabunge wa chama cha African Patriots of Senegal for Work, Ethics, and Fraternity (PASTEF) walijaribu kumwondoa kwa nguvu, na kusababisha mvutano mkali. Polisi hatimaye waliingilia kati kwa amri ya Ousmane Sonko ya kumwondoa kwenye chumba cha mikutano. Wabunge wa upinzani walilaani mara moja hili kama unyakuzi wa madaraka na wakaamua kususia kikao hicho.

Baada ya kura ambapo marekebisho yote ya serikali yalikataliwa, Spika wa Bunge la taifa alitangaza nia yake ya kumwomba Rais wa Jamhuri mara moja kuidhinisha rasimu hiyo kama yalivyo, na hakusita kutoa maneno dhidi yake: “Katiba si ya Bassirou Diomaye Diakhar Faye. Ni kwa misingi gani mtu mmoja anaweza kujipa mamlaka ya kuchagua ni vifungu vipi vinavyomfaa na vipi visivyomfaa?” “Hiki ndicho kila kitu ambacho PASTEF imepambana kwa miaka kumi, pamoja na nguvu zote ambazo zimetumiwa, na ambazo rais alitaka kuzikanyaga,” alisema Ousmane Sonko.

Kupitia sauti ya Waziri wa Sheria, Moussa Sarr, Bassirou Diomaye Faye alionyesha kwamba rasimu ya mageuzi ya katiba itawasilishwa kwa kura ya maoni, bila kutangaza tarehe—mtazamo ambao tayari unazua wasiwasi, ikizingatiwa kwamba uchaguzi umepangwa kufanyika mwezi Januari mwakani.

Je, mageuzi yameundwa kwa ajili ya Ousmane Sonko?

Kulingana na wapinzani wa rasimu hii—muungano wa Diomaye Rais, vyama kadhaa vya upinzani, na mashirika ya kiraia—suluhisho hili, pamoja na kupelekwa kwa suala hilo kwa Baraza la Katiba na mkuu wa nchi mwenyewe au na moja ya kumi ya wabunge, lilikuwa mojawapo ya njia mbili zinazowezekana za kuzuia mageuzi hayo.

Hata hivyo, kuandaa mashauriano kama hayo kunaibua matatizo kadhaa, hasa yale ya vifaa na kifedha, kama ilivyoelezwa na Mbunge huru wa upinzani Thierno Alassane Sall: “Chama cha PASTEF kinakusudia kulifanya Bunge la taifa kuwa na nguvu ya kukabiliana na Rais wa Jamhuri, ambaye hana chaguo lingine ila kuitisha kura ya maoni. Na hilo ni jambo la kusikitisha,” alisema kabla ya kuendelea: “Je, Senegal inaweza kumudu anasa ya mashauriano kama hayo na gharama zote zinazohusiana wakati vipaumbele vingine viko mbele na kalenda ya uchaguzi tayari imebeba mzigo mkubwa?”

Ikiwa kura ya maoni itafanyika, kampeni zinaweza kukumbwa na na wasiwasi” ,  amesema Maurice Soudieck Dione, Profesa Mshiriki wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Gaston Berger huko Saint-Louis

Kimsingi, rasimu hii inarekebisha vifungu 29 vya Katiba na inafafanua upya uwiano wa madaraka: inamkataza Rais wa Jamhuri kuongoza chama cha siasa, inaimarisha mamlaka ya Bunge la taifa na Waziri Mkuu, inabadilisha Baraza la Katiba na Mahakama ya Katiba inayoundwa na wajumbe tisa, na inaweka kikomo cha kuvunjwa kwa Bunge mara moja kwa muhula wa rais.

Wapinzani wanabaini rasimu hii ilitengenezwa mahususi kwa ajili ya Ousmane Sonko, aliyeachishwa kazi kama Waziri Mkuu mwezi mmoja uliopita na sasa ni Spika wa Bunge la taifa. Wapizani hawa pia wanatoa wito wa mashauriano zaidi.

Chama cha PASTEF, kwa upande wake, kinajibu kwamba vifungu hivyo vinatokana na mazungumzo ya kitaifa ya mwaka 2025 na Mkutano wa Kitaifa wa Haki wa mwaka 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *