Picha ya rais Putin

Chanzo cha picha, GETTY

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 4

Rais wa Urusi Vladimir Putin amekuwa akisisitiza kuwa vikosi vya Urusi vimezidi kupiga hatua katika mstari wa mbele wa vita nchini Ukraine.

Putin katika mahojiano alisema kuwa tayari wamedhibiti eneo la Konstantinovka na Lyman akiichanganya na eneo la Oskol huku pia wakilenga kudhibiti mji wa Sumy.

Ila semi za Putin zinakinzana na ripoti ya waangalizi huru. Mapigano bado yanaendelea eneo la Kostyantynivka, eneo la Lyman bado linadhibitiwa na vikosi vya Ukraine na mji wa Sumy na mto Oskol bado haujazingirwa kama anavyodai Putin.

Hii si mara ya kwanza rais Putin amewamiminia sifa za kupitiliza vikosi vya Urusi kwa kudhibiti maeneo ya Ukraine.

Tarehe 12 mwezi Juni, kiongozi huyo alisema majeshi ya Urusi yanakaribia eneo la Zaporizhia

Lakini nyaraka kutoka Jeshi la 58 na data kutoka kwa watafiti huru zinaonyesha kuwa ramani za Kamandi Kuu ya Jeshi la Urusi katika eneo hili zinaweza kutofautiana na hali halisi kwa makumi ya kilomita, jambo ambalo linaweza kuwa na madhara ya mauti kwa wanajeshi wa Urusi wanaofanya kazi katika eneo hilo.

Shirika la BBC la Urusi lilichunguza nyaraka za kijeshi na kugundua jinsi jeshi linavyopigana huku mtazamo wao kuhusu mstari wa mbele wa vita ukiwa hauendani na uhalisia.

.

Chanzo cha picha, Alexander Kazakov/SPUTNIK/KREMLIN/EPA/Shutterstock Location

Ripoti zisizokuwa na udhibitisho

Tarehe 12 mwezi Juni baada ya kutoa tuzo za “Mashujaa wa Kazi” na tuzo nyingine za serikali, Rais wa Urusi Vladimir Putin alikutana na kikosi cha mashambulizi cha jeshi la Urusi. Rais alizungumza na mmoja wao ambaye alimwambia

“Kwa kutumia beji hii ya kikosi chetu, tuliteka makazi ya Kamianske na Stepovoe katika eneo la Zaporizhia mwaka jana, na tunaamini hii ni zawadi yetu ndogo kwako,” alisema Luteni Sergey Chuvashov, kamanda wa kikosi cha paratroopers kutoka kikosi cha 247, akimkabidhi rais huyo beji hiyo.

“Hili ni kundi la Dnipro, sivyo?” Putin aliuliza?

“Mnazidi kusogea kuelekea Zaporizhia?”

“Hongereni.”

Kauli hii ilizua mshangao mkubwa kwa kila upande kuanzia wataalamu huru wa masuala ya kijeshi hadi waandishi wa mitandao ya “z-channels” kwa kuwa jeshi la Urusi halijafika hata karibu na Zaporizhia.

Jeshi la Urusi halijaweza kufikia mji huo, ambao Vladimir Putin aliutangaza kuwa kama sehemu ya Urusi mnamo mwezi Oktoba mwaka wa 2022 .

Ila hali ni tofauti sana. Mashambulizi ya jeshi la Urusi katika eneo hilo yalisimama miezi kadhaa iliyopita, huku vikosi vya Ukraine vikiwa vimefanikiwa kurejesha udhibiti wa Stepnohirsk kijiji kilicho kaskazini kidogo mwa Kamianske pamoja na kuikomboa baadhi ya maeneo kwenye mpaka wa mikoa ya Dnipropetrovsk na Zaporizhia.

Eneo la Sumy

Hii ni sehemu ya mstari wa mbele wa vita katika eneo la Zaporizhia, kulingana na Taasisi ya Marekani ya Utafiti wa Vita (ISW) kufikia Juni tarehe 13, mwaka wa 2026.

Ripoti ya taasisi hiyo inaonyesha makazi yale yale ya Kamianske na Stepove, ambayo, kulingana na Luteni Chuvashov aliyezungumza na Putin, yalitekwa kwa mashambulizi na kikosi chake mwaka jana.

Hata hivyo, kulingana na ramani za makao makuu na nyaraka zinazoambatana za Jeshi la 58, inaelezea kuwa vikosi vya Urusi vilikuwa vimeondoka eneo hilo muda mrefu uliopita, baada ya kusonga mbele kilomita 16 hadi 20 ndani ya ardhi ya Ukraine kuelekea kaskazini.

Taarifa rasmi za upande wa Urusi zinaendana na ramani za makao makuu, ambazo zinaonyesha kuwa jeshi linaendesha mapigano moja kwa moja lakini yote haya yanatofautiana sana na hali halisi ya nyanjani.

.

Chanzo cha picha, Deepstate

Kulingana na majenerali wa Urusi, makazi ya Richne yako chini ya udhibiti thabiti wa vikosi vyao.

Belousov pia aliwapongeza askari wa Kikosi cha 247 kwa “kuteka” Veselyanka tarehe 4 mwezi Machi. Aidha, kuhusu kutekwa kwa Tokmachka, kijiji kidogo katika eneo la Zaporizhia ,Waziri wa Ulinzi wa Urusi Andrei Belousov aliwapongeza wanajeshi wa Divisheni ya 42 kwa kukiteka kijiji hicho.

Hata hivyo, kulingana na watafiti huru wa masuala ya kijeshi na picha za setilaiti, kufikia mwezi Juni 2026, vikosi vya Urusi havikuwa vimeuteka kijiji hicho.

Taarifa za hivi karibuni kutoka Wizara ya Ulinzi ya Urusi ni kuwa vikosi vyao vimeteka maeneo kadhaa ya Zaporizhia.

.

Chanzo cha picha, Russian Defence Ministry Press Service Handout/EPA/Shutterstock

.

Chanzo cha picha, Reuters

Uvamizi maarufu zaidi katika historia ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ulifanywa na kamanda wa kikundi cha “West”, Jenerali Sergey Kuzovlev. Mwishoni mwa mwaka wa 2025, aliripoti kwa Vladimir Putin kwamba wanajeshi wa kikundi chake walikuwa wamekamilisha mashambulizi ya Kupyansk na kuichukua kikamilifu chini ya kuudhibiti, jambo ambalo lilimletea tuzo ya “Shujaa wa Urusi”.

Hata hivyo, kwa uhalisia, hali ilikuwa kinyume kabisa. Wanajeshi wa Urusi waliondolewa na wanajeshi wa Ukraine na eneo hilo liko chini ya udhibiti wa vikosi vya Ukraine.

Mashambulizi yasiyo na mwisho

Tangu mwaka wa 2022, baada ya kushindwa kwa jeshi la Urusi mashariki mwa Kharkiv, mwanahistoria wa Uingereza na mtaalamu wa masuala ya kijeshi Chris Owen alibainisha kwamba maafisa wa jeshi la Urusi mara nyingi huwadanganya wakuu wao kuhusu hali halisi ya mambo na hali ya vitengo vyao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *