Baadhi ya wanawake wafanyabiashara wadogo wanaouza mbogamboga katika Soko la Majengo, jijini Dodoma, wameipongeza Serikali kwa uamuzi wa kusitisha mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, wakisema hatua hiyo itasaidia kulinda amani na kuzuia vurugu zinazoweza kuathiri shughuli zao.
Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa wafanyabiashara hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Winfrida, amesema uamuzi huo umeleta matumaini kwa wafanyabiashara wadogo ambao hutegemea biashara za bidhaa zinazoharibika haraka kama nyanya na mboga mboga.
Amesema bado anakumbuka athari zilizotokana na matukio ya Oktoba 29, ambapo wafanyabiashara wengi walipata hasara kubwa na kupoteza mitaji.
Ameeleza kuwa wengi wao wana mikopo ya kurejesha, watoto wanaohitaji nauli na mahitaji ya shule kila siku, huku baadhi yao wakiwa walemavu au wagonjwa waliopata athari kubwa kutokana na kusimama kwa biashara.
(Feed generated with FetchRSS)