
DAR ES SALAAM; SHANGWE la ubingwa. Yanga wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2025/26 kufuatia ushindi wa mabao 0-3 walioupata leo dhidi ya JKT Tanzania mchezo wa mwisho Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kutokana na ushindi wa mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Yanga imemaliza ligi ikiwa na pointi 75 ikifuatiwa na Simba yenye pointi73, ambayo yenyewe imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.
Yanga, mabingwa watetezi wa kombe hilo kwa misimu minne mfululizo leo ilikuwa inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote kutangaza ubingwa huo na hivyo kuutetea kwa mara ya tano mfululizo.