Raia wa DRC waishio nchini Kenya wameitaka Jumuiya ya kimataifa na ile ya kikanda kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa amani ya mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika kongamano la vijana lililoandaliwa katika muktadha wa maadhimisho ya miaka 66 ya Uhuru wa DRC, mwenyekiti wa Wakongomani waishio nchini Kenya François Alwende amezitaka jumuiya ya kimataifa na kikanda kuja na kauli moja kuhusu mustakabali wa DRC.

‘‘Tunaomba nchi zengine, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kiraia yapate kuisaidia serikali ya Congo na zaidi raia wa Congo wapate amani.’’ Alisema François Alwende.

Dkta Raymond Danga afisa katika Umoja wa Afrika, amesema raia wa Congo wanakabiliana na shida za mara kwa mara, kwenye mipaka ya nchi za afrika mashariki.

‘‘Kwanza DRC ilikaribishwa vizuri na tumefurahia kuwa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ila sisi Wakongomani tunakabiliwa na changamoto ya kuingia na kuondoka ambapo tunataka hilo liangaziwe.’’ Alisema Dkta Raymond Danga.

Naye Baraka Mwamba mmoja wa watafiti kuhusu usuluhishi wa migogoro amewataka raia wa Congo kuitetea nchi yao.

‘‘Bado kuna mambo ambayo yanathibitisha kwamba Congo bado hijapata uhuru wake. Kwa sababu huwezi kusema kwamba kuna uhuru wakati nchi iko kwenye vita.’’ Alisema Baraka Mwamba.

DRC, Jumatano ya wiki hii iliadhimisha miaka 66, uhuru kutoka kwa mkoloni wake Ubelgiji, sherehe zilizogubikwa na hali tete ya usalama mashariki mwa nchi hiyo pamoja na mlipuko wa Ebola.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *