Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi anaowateua kubeba dhamana walizopewa na wathibitishe kwa kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kuleta matokeo yanayoonekana kwa wananchi.
Rais Samia ameyasema hayo, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatano Julai 1, 2026, alipozungumza baada ya kuwaapisha viongozi kadhaa aliowateua hivi karibuni.
“Heshima au dhamana mliyopewa leo sio vyeo tu, kwamba mmebeba vyeo, lakini ni dhamana ambayo inatakiwa ikafanyiwe kazi,” amesema.
Amesema wateule hao wameapa siku ambayo wanapaswa kuanza kazi kwani ndipo utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unapoanza rasmi.
“Mjue kwamba mnaingia si kwenda kupumzika kwamba nimepata cheo ngoja ni-relax, bali mnaingia kwenye mchakamchaka wa kweli kweli kwa sababu Dira hii lazima tuitekeleze kwa kasi,” amesema Rais Samia.
(Feed generated with FetchRSS)