• Mchungaji Kanyari alidai watoto wake walirejea kuishi na baba yao wa kambo, Tash, baada ya hivi karibuni kusema alikuwa amepata tena ulezi wao
  • Mhubiri huyo alidai shule ya watoto hao haimtambui rasmi kama baba yao licha ya juhudi zake za kutaka kumbukumbu za shule zibadilishwe
  • Nyaraka zilizovuja kutoka shuleni pamoja na stakabadhi za malipo ya karo zilionekana kumtaja Tash kama mzazi anayetambuliwa rasmi, jambo lililochochea mjadala mpya kuhusu mzozo wa ulezi

Mchungaji Victor Kanyari ametoa madai mapya katika mzozo unaoendelea wa ulezi wa watoto wake, akidai kuwa shule yao haimtambui rasmi kama baba yao.

Pastor Kanyari and Tash posing for a photo during Betty Bayo's burial.
Pastor Victor Kanyari shared an update regarding his ongoing custody dispute with Tash over his children. Photo: Karangu Muraya.
Source: Facebook

Kauli za mhubiri huyo zimezua mjadala mpya mtandaoni, siku chache tu baada ya kudai kuwa alikuwa amepata tena ulezi wa watoto wake wawili kabla ya baadaye kusema walirejea kuishi na baba yao wa kambo, Hiram Gitau, anayefahamika zaidi kama Tash.

Kwa nini Kanyari na Tash wanatofautiana?

Kanyari alidai kuwa watoto wake, Sky Victor na Danivictor, wamerudi nyumbani kwa Tash baada ya kuishi naye kwa muda mfupi.

Pia soma

Risiti Zavuja! Kiasi Halisi Kilicholipwa Kumsajili Sky Woodcreek Chafichuliwa

Watoto hao wawili wamekuwa wakiishi na Tash katika nyumba yao ya Edenville Estate tangu kifo cha mama yao, Betty Bayo, mwezi Novemba mwaka jana.

Tangu Betty alipofariki, Kanyari amekuwa akieleza mara kwa mara kuwa anatamani watoto hao waishi naye. Hata alinunua nyumba mpya Runda, akisema alitaka kuwapa mwanzo mpya. Hata hivyo, suala hilo limeendelea kuwa na mvutano.

Hivi karibuni, Kanyari alidai kuwa alikuwa amenyimwa nafasi ya kuwaona watoto wake na pia akadai karo yao haikuwa inalipwa, jambo lililomsukuma kudai apewe ulezi kama baba yao wa kuwazaa.

Siku chache baadaye, alitangaza kuwa alikuwa amepata tena ulezi wa watoto hao, lakini baadaye akadai walikuwa wamerudi kuungana na Tash.

Kwa nini Kanyari anasema shule haimtambui?

Akizungumza kupitia mahojiano ya simu na mwanablogu Shiru wa Oakland, Kanyari alidai kuwa Betty alikuwa amejiandikisha yeye mwenyewe pamoja na Tash kama wazazi wa watoto hao katika rekodi za shule.

Kulingana na mhubiri huyo, alifika shuleni akitarajia rekodi hizo zirekebishwe, lakini juhudi zake hazikufanikiwa.

“Betty Bayo alikuwa ameandika yeye na…” alisema Kanyari alipokuwa akieleza ni nani shule inawatambua rasmi kama wazazi wa watoto hao.

Pia soma

Kanyari Afunguka Baada ya Kudai Kushinda Vita vya Ulezi wa Watoto Wake

Aliongeza kuwa suala hilo sasa liko mahakamani, huku kesi hiyo ikitarajiwa kusikilizwa Ijumaa, Julai 3.

Licha ya mzozo unaoendelea, Kanyari alisema hataki drama zisizo za lazima zinazowahusu watoto wake na ana matumaini kuwa suala hilo litapatiwa suluhisho kupitia mchakato wa kisheria.

Tazama video hapa chini:

Shule inamtambua nani?

Madai mapya ya Kanyari yanajiri muda mfupi baada ya nyaraka za shule na stakabadhi za malipo ya benki zinazohusiana na shule ya Sky kuvuja mtandaoni.

Nyaraka hizo zilionekana kuonyesha Betty na Tash kama wazazi wanaotambuliwa rasmi, huku mawasiliano ya shule yakielekezwa kwao.

Stakabadhi zilizovuja pia zilionyesha kiasi kikubwa cha karo kilicholipwa na Tash. Nyaraka hizo zilianza kusambaa baada ya madai kuenea mtandaoni kuwa Kanyari ndiye alikuwa akilipa karo ya watoto hao huku akidaiwa kunyimwa nafasi ya kuwaona.

Wanamtandao wachangia mjadala

Maendeleo hayo mapya yamezua mjadala mkubwa mtandaoni, huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakiendelea kutoa maoni kuhusu mgogoro huo wa kifamilia.

Haya ni baadhi ya maoni yao:

Caroline Ng’ang’a:

“Sielewi kwa nini Tash anafanya hivi.”

peninahmulandi:

“Jumapili itawahi fika tukunywe hii chai. Betty alikuwa ameandika yeye naaa… Ninataka kusikia mahali hapo, inaonekana kama kuna mengi ambayo hatujui.”

Pia soma

Kanyari apiga abautani, akubali kushirikiana na Tash kuwalea watoto lakini kwa masharti mazito

Hannah:

“Ningependa watu waelewe kwamba haihusu jinsi wanavyostarehe au uhuru wao… inahusu uhalisia wa maisha, endapo maisha yakienda mrama, matatizo ya kiafya, je bado watakuwa na baba yao?!!! Kama hawezi kulipa ada za shule, itakuwaje na maisha magumu zaidi ya hayo?”

rozy:

“Kanyari: Mimi sitaki maigizo.”

Tash na Sky Victor wakipozi kwa picha.
Kufuatia kifo cha mama yao, Betty Bayo, Sky na Danivictor wamekuwa wakiishi na baba yao wa kambo, Tash. Picha: Sky Victor.
Source: TikTok

Je, Mchungaji Kanyari yuko tayari kulea watoto pamoja na Tash?

Hapo awali, Mchungaji Kanyari alisema alikuwa tayari kushirikiana na Tash katika kulea watoto hao, ingawa alisisitiza kuwa wanapaswa kuhamia nyumbani kwake Runda.

Alisema hana chuki yoyote dhidi ya Tash, akieleza kuwa kipaumbele chake ni kujenga upya uhusiano wake na watoto wake na kushiriki kikamilifu katika maisha yao.

Kanyari pia alizungumzia ndoto za binti yake Sky kuhusu maisha yake atakapofikisha umri wa miaka 25.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *