DAR ES SALAAM; BUNGE la Tanzania linatarajia kufanya maadhimisho ya miaka 100 ya chimbuko la bunge hilo.
Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo Julai Mosi, 2026 na Spika wa Bunge hilo, Mussa Azzan Zungu kwenye mkutano maalumu na wahariri kuhusu maadhimisho hayo.
Amesema wanachoangalia ni chimbuko la bunge hilo kuanzia lilipoanzishwa Machi 19, 1926, wakati nchi ikiitwa Tanganyika ikiwa koloni la Uingereza, hadi ilipopata uhuru mwaka 1961 na baadaye kuungana na Zanzibar na kuzaliwa Tanzania mwaka 1964.
Amesema bunge la ukoloni lilizinduliwa rasmi Oktoba 10, 1926 na kuanza kufanya kazi zake Desemba mwaka mwaka huo na kueleza kuwa matukio mbalimbali yatafanyika katika maadhimisho ya miaka hiyo 100 na kilele chake kitakuwa Januari 2027.
