Serikali imetangaza kuanza kutoa vibali vya ujenzi na kufanya mazungumzo na wamiliki wa ardhi na nyumba walio tayari kushiriki katika Mpango wa Uendelezaji Upya wa eneo la Sinza, huku ikifuta mchakato uliopita ili kuanza upya kwa uwazi na ushirikishwaji wa wananchi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo, amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya baadhi ya wananchi kulalamikia mchakato wa awali, hivyo mazungumzo mapya yatafanyika kwa lengo la kujenga maridhiano.
Dkt. Akwilapo amesema ukuaji wa miji unalazimu Serikali kupanga matumizi ya ardhi ili kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye, akibainisha kuwa Sinza imebadilika na inahitaji mpango mpya wa maendeleo unaoendana na hadhi yake.
Amesema maeneo kama Posta, Kariakoo, Upanga, Oysterbay na Masaki yalinufaika na uendelezaji upya, na kusisitiza kuwa mpango wa Sinza unalenga kuboresha makazi, biashara na miundombinu kwa manufaa ya wananchi.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)