.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 3

Japan imeweka rekodi mpya ya watu waliozidi umri wa miaka 100 na kufikia karibu watu 100,000, kulingana na takwimu ya serikali ya nchi hiyo.

Japan imeshikilia rekodi hii kwa miaka 55 mfululizo, mwaka wa 2025, Japan ilikuwa na watu 99,763 waliokuwa na zaidi ya umri wa miaka 100.

Asilimia 88 ya watu hao waliozidi umri wa miaka 100 ni wanawake.

Mwaka wa 2025 Waziri wa afya wa wakati huo, Takamaro Fukoka, aliwapongeza wanawake 87,784 na wanaume 11,979 waliovuka umri wa miaka 100, na kusema kuwa “shukrani kwa miaka yao mingi ya mchango katika maendeleo ya jamii.”

Japan inatoa fursa ya muda wa kuishi zaidi duniani na mara nyingi hujulikana kama nchi inayohusishwa na watu wazee zaidi duniani, ingawa baadhi ya tafiti zinatilia shaka takwimu za watu wenye umri wa zaidi ya miaka 100.

Mtu mzee zaidi nchini Japan ni Shigeko Kagawa, mwanamke mwenye umri wa takribani miaka 115 kutoka Yamatokoriyama, kitongoji cha jiji la Nara. Mzee zaidi wa kiume ni Kiyotaka Mizuno, mwenye miaka 112, mkazi wa Iwata, jiji la pwani.

Takwimu hizi zilitolewa kabla ya Siku ya Wazee ya Japan, inayoadhimishwa tarehe 15 Septemba ambayo huwa likizo ya kitaifa, ambapo watu waliovuka miaka 100 hupokea barua ya pongezi na kikombe cha fedha kutoka kwa waziri mkuu.

Mwaka wa 2025, watu 52,310 walistahiki kupokea heshima hiyo, kulingana na wizara ya afya.

Karibu miaka ya 1960, Japan ilikuwa na kiwango cha chini zaidi cha watu wenye umri wa zaidi ya miaka 100 miongoni mwa nchi za G7, lakini hali hii imebadilika sana tangu wakati huo.

Wakati serikali ilipoanza kufanya utafiti wa watu wenye miaka 100 mwaka 1963, kulikuwa na watu 153 pekee waliokuwa na umri huo au zaidi.

Idadi hiyo iliongezeka hadi 1,000 kufikia 1981, na ikafikia 10,000 kufikia 1998.

Kuongezeka kwa muda wa kuishi kunahusishwa zaidi na kupungua kwa vifo vinavyotokana na magonjwa ya moyo au aina za kawaida za saratani, hasa saratani ya matiti na ya tezi dume.

Japan ina viwango vya chini vya unene wa kupindukia, jambo ambalo huchangia magonjwa haya, wao hua mlo wenye mafuta kidogo ya nyama nyekundu na wenye mboga na samaki kwa wingi.

Viwango vya unene wa kupindukia ni vya chini hasa kwa wanawake nchini Japan, jambo ambalo linaweza kuelezea kwa kiasi fulani kwa nini wana muda mrefu zaidi wa kuishi kuliko wenzao wa kiume.

Japan pia iliendesha kampeni ya kuwahamasisha watu kupunguza kiwango cha chumvi wanachotumia.

Hata hivyo, si suala la lishe pekee. Raia wa Japan hufanya mazoezi kwa kutembea kwa miguu na kutumia usafiri wa umma wakati mwingi.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hata hivyo, tafiti kadhaa zimeweka mashaka kuhusu uhalisia wa idadi ya watu wanaozidi umri wa miaka 100 na zaidi.

Utafiti umeonyesha kuwa makosa ya uchakataji wa data, nyaraka rasmi zisizo sahihi, au ukosefu wa vyeti vya kuzaliwa huenda vilichangia idadi kubwa iliyoripotiwa ya watu walio na umri wa miaka 100 au zaidi.

Ukaguzi wa serikali wa mwaka 2010 kuhusu kumbukumbu za familia nchini Japani ulifichua kuwa zaidi ya watu 230,000 walioripotiwa kuwa na umri wa miaka 100 walikuwa hawapatikani tena, na walikuwa wamekufa miongo kadhaa iliyopita.

Makosa hayo ya uhasibu yalihusishwa na data za idadi ya watu ambazo hazikuwahi kuhakikiwa, pamoja na mashaka kwamba baadhi ya familia huenda zilificha vifo vya wazee wao ili kuendelea kupokea marupurupu yao ya uzeeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *