Polisi tayari wametangaza uchunguzi kuhusu kifo cha raia wa kigeni ambaye inasemekana alianguka na kufa kutoka kwenye jengo huko Durban, ikiamini alikuwa akikimbizwa. Ingawa polisi walifanikiwa kuzuia mbaadhi ya misafara ya waandamanaji, matukio mengi yalitokea kote nchini, na vurugu hizi za chuki dhidi ya wageni hazijaisha, kwani vuguvugu la “March and March” linapanga kufanya maandamano kila Alhamisi ili kuendelea kuishinikiza serikali.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu jijini Johannesburg, Valentin Hugues

Kwa jumla, takriban maandamano 300 ya kupinga uhamiaji yalifanyika Afrika Kusini siku ya Jumanne. Siku moja baada ya maandamano hayo, Luteni Jenerali Tebello Mosikili amevipongeza vikosi vya usalama kwa kuzuia machafuko.

“Ingawa kulikuwa na visa vya uhalifu, vya watu waliotaka kutumia vibaya hali hiyo, vitendo vyao havikuhatarisha utulivu wa jumla wa nchi. Zaidi ya watu 900 walikamatwa wakati wa operesheni zilizofanywa siku ya Jumanne. Wengi wa waliokamatwa ni wahamiaji wasio na vibali. Wengine walikamatwa kwa vurugu za umma au uharibifu. Na maeneo yaliyoathiriwa yanafuatiliwa kila mara.”

Katika kitongoji tete cha Hillbrow cha Johannesburg, kwa mfano, ambapo hali ilizidi kuwa mbaya haraka, jeshi, likisaidia polisi, lililazimika kuingia mitaani, hasa baada ya kuripotiwa kwa milio ya risasi. “Ninaweza kuthibitisha kwamba watu wawili walikuwa wahanga wa jaribio la mauaji lililohusisha milio ya risasi; kamata kamata ilifuatia tukio hili, ambalo lilitokea siku ya Jumanne yapata saa 2:30 usiku.”

Licha ya picha za maduka yaliyovamiwa, kwa sasa, matukio hayajawa kama ya mwaka 2008, ambapo vurugu za chuki dhidi ya wageni zilisababisha vifo vya watu 62. Lakini waandamanaji wanaopinga wahamiaji sasa wanapanga kuingia mitaani kila Alhamisi, na vikosi vya usalama vinaendelea kuwa macho.

Polisi kwa sasa wanafanya uchunguzi wa mauaji katika mji wa Alexandra huko Johannesburg, kufuatia kupigwa risasi kwa kijana mmoja “usiku wa Juni 30.” “Karibu saa 2 mchana, inaripotiwa wakazi walianza kupora maduka yanayomilikiwa na raia wa kigeni wakati risasi zilipofyatuliwa, na kumjeruhi mwathiriwa mmoja,” polisi imesema katika taarifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *