- Mwanamke mmoja Mkenya alizua mjadala mtandaoni baada ya kuwaonya wanaume dhidi ya kula mara kwa mara chapo madondo
- Nola Herbalist alieleza sababu za madai yake na kuwashauri wanaume kuhusu vyakula wanavyopaswa kula badala yake
- Kauli zake zilisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii huku Wakenya wengi wakizitilia shaka na kupinga madai yake kuhusu lishe
Mwanamke mmoja Mkenya amezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuwaonya wanaume dhidi ya kula chapati na maharagwe kwa wingi.

Source: TikTok
Nola Herbalist, kupitia video ya TikTok, alidai kuwa mlo maarufu unaojulikana kama chapo madondo si chaguo zuri kwa afya ya wanaume.
Alisema watu wengi wamejikita katika kutafuta pesa badala ya kutunza afya zao, akiongeza kuwa mwili hatimaye “utalalamika” unapopuuzwa.
“Chapo madondo si chakula cha mwanaume. Chakula hicho kitaharibu mwili wako kama mwanaume. Najua kinapatikana kwa urahisi, lakini epuka kukila kwa sababu kinakudhuru kwa njia ambazo huwezi kuziona. Ndiyo maana baadhi ya wanaume hawawezi kutimiza wajibu wao wa ndoa, wanapata maambukizi ya njia ya mkojo, kisukari na magonjwa mengine mengi,” alidai.
Kwa mujibu wa Nola, lishe ina athari ya moja kwa moja kwa afya na ustawi wa mtu kwa ujumla.
Aliwashauri wanaume waepuke kula vyakula vya wanga kwa wingi, hasa wale ambao hawafanyi shughuli nyingi za kimwili.
Aliendelea kudai kuwa chapo madondo haina thamani kubwa ya lishe, akidai kuwa chapati ina kemikali zinazowafanya wanaume “kuwa kama wanawake” taratibu.
“Chapati ina gluten, ambayo hupunguza kiwango cha testosterone, homoni ya kiume inayokufanya uwe mwanaume. Kadiri unavyokula chapati nyingi, ndivyo kiwango chako cha testosterone kinavyopungua. Protini iliyoko kwenye maharagwe ni kidogo sana na haiwezi kulinganishwa na ile ya nyama,” alidai.
Nola aliwashauri wanaume wale mboga za majani kwa wingi pamoja na omena na kiasi kidogo cha ugali, akisema ni muhimu kuchukua hatua mapema kulinda afya.
Pia alidai kuwa mwanaume anayekula mboga nyingi atakuwa na nguvu zaidi na afya bora kuliko anayekula chapati na maharagwe kwa wingi.
Wakenya waijibu kauli kuhusu chapo madondo
Wakati baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii waliomba kupendekezewa vyakula mbadala vyenye afya, wengine walipuuza kauli zake wakisema wamekula chapo madondo kwa miaka mingi bila kupata madhara aliyoyataja.
KRAUSE DANIELS 254:
“Haijalishi unakula chakula cha afya kiasi gani, mwisho wa siku sote tutakufa. Sioni maana ya kula chakula kisicho na ladha kikiitwa chakula cha afya.”
Jemo:
“Wewe huwa unakula nini kwa kawaida? Tafadhali tupe mbadala.”
Chwani:
“Niaje mtu wangu. Dengu vipi? Nimekuwa nikifikiria ni alkaline baada ya kumeng’enywa. Ama zimejaa wanga kama maharagwe?”
Damkey:
“Wee acha, tumekula hadi tumezeeka na bado hatujawa watu wasioweza kutekeleza majukumu ya ndoa. Nusu ya dunia inaishi kwa ngano, nusu nyingine kwa mchele. Mwisho wa siku, ukweli ndio huo ninaouona.”
Bismarck:
“Mafuta ya mbegu, sukari, mafuta mengi, nyama, mayai na mafuta ndiyo adui. Mimea si adui.”
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke

